WAWILI WAJERUHIWA MAPANGA.



WAWILI WAJERUHIWA MAPANGA.

 BARIADI

Watu wawili wamevamiwa na kujeruhiwa kwa mapanga  na watu wasiofahamika katika kijiji cha Ditima kata ya Guduwi  wilayani Bariadi Mkoani Simiyu na kukatwakatwa  mapanga kisha watu hao kutokomea kusikojulikana.

Akiongelea  tukio hilo ,esther  jali ambaye ni mmoja wa  majeruhi   alisema  majira ya saa moja usiku wa kijiandaa kula chakula na mama yake , ghafla walivamiwa na watu wasiofahamika na kuanza kushambuliwa.


Walianza kumkata mama kikongwe mwenye umri wa miaka 80 kichwani na shingoni ,kisha kumkata panga binti yake mkono wa kulia, wakati  akijaribu kumsaidia mama yake kwa kelele za kuomba msaada   watu hao walitoweka eneo hilo.

Naye  kijana wa mama huyo  Daudi Kabale  alisema alisikitishwa sana  na kitendo hicho cha kikatili ambacho kinawaweka wakinamama katika hali ya wasiwasi na kuiomba serikali kuingilia kati suala hilo.

Kwa upande wake mganga wa zamu ktk hospitali ya wilaya ya bariadi Revocatus Nkumbi alikiri kupokea majeruhi hao , wakati mmojawapo akiwa ameishiwa damu kutokana na kuvuja damu nyingi ,hivyo juhudi za kuyaokoa maisha yake zimefanikiwa.

“Tulipokea majeruhi hao wawili hospitalini hapa na harakati za kuokoa maisha yao zinaendelea kufanyika ili kuyanusuru maisha yao”, alifafanu mganga Nkumbi.

Kaimu  kamanda wa polisi wa mkoa wa simiyu  Venance Kimario alithibitisha kutokea kwa tukio lilo na kwamba uchunguzi  wa kuwasaka watu hao unaendelea ili kuwafikisha mahakamani juu ya tukio hilo.

Powered by Blogger.