Tarime watakiwa kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia:
Vijana wakitoa Maigizo yenye ujumbe kuhusu madhara yatokanayo na hathari za ukeketaji, Ndoa za utotoni, pamoja naMimba za utotoni katika tamasha la kupinga ukatili wa kijinsia lililoandaliwa na TGNP mtandao hivi karibuni na kufanyika katika shule ya msingi Ng'ereng'ere kata Nyamaraga wilayani Tarime Mkoani Mara takribani siku tatu huku zikijadiliwa mada mbalimbali kwa lengo la kubadilisha jamii.
Tarime watakiwa
kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia:
Jamii imetakiwa kufichua vitendo vya ukatili vinavyozidi
kutendeka maeneo mbalimblai wilayani humo kwa serikali, Taasisi za watu
binafsi,mashirika kwa lengo la kutokomeza vitendo hivyo.
Kauli hiyo imetolewa na Ofisa tawala Bw: Baraka Nyamsenda
kwa niaba ya mkuu wa wilya ya Tarime John Henjewele katika ufunguzi watamasha
la kupinga ukatili wa kijinsia, Ukeketaji, Ndoa za utotoni lililofanyika katika shule ya msingi ng’ereng’ere kata Nyamaraga wilayani Tarime Mkoani Mara.
Mgeni rasmi alisema kuwa jamii kwa ujumla iondokanae nasuala
la kuwaficha wale wanausika katika kutenda unyama kwa wakina mama, watoto wa
kike kwa kushirikiana na serikali ili
kuweza kuwachukulia hatua mara moja na kutokomeza vitendo vya kikatilia
wilayani Tarime.
“Siri mlizonazo ndo zinazidi kutupa changamoto kwa mashirika
Halmashauri kwakushirikiana na mkuu wa wilaya tupo bega kwa bega kupinga
vitendo hivyo” alisema mgeni rasmi.
Merry msemwa ni meneja wa
programu katika uanarakati,
Utafiti na Ushawishi pamoja na Utetezi katika TGNP Mtandao katika tamasha hilo
alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa tamasha hilo ambalo litachukua takiribani
siku tatu nikuweka mikakati mahususi ili kila mtu kuweza kupata fursa ya
kushiriki tamasha hilo na kutoa mawazo yake.
“Matamasha haya tumekuwa tukiyafanyia Dar –es salaam lakini
mwaka huu tumeamua kufika kwa walengwawenyewe wanaokumbwa na masula ya ukatili
wa kijinsia” alisema Mery.
Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za
wanawake la kivulinilililo po jijini
mwanzaBi: Maim una Kanyamala katika
kutoa mada halisi juu yua ukeketaji na ndoa za utotoni mbele ya mgeni rasmi alisema kuwa wameamua
kuongelea mada hiyo kwa sababu wanajali utu wa jamii nzima bila kujali umri, elimu,dini,na itikadi ya vyama.
Aliongeza kuwaMkoa wa mara ni kati ya mikoa mitatu nchini inayoongoza
kwa kiwango kikubwa sana katika ndoa za utotoni, nakusema kuwa
takwimu za kitaifa zinaonesha zaidi ya nusu ya wasichana wadogo wanaozwa. Mikoa
mongine ni Shinyanga asilimia59% Taboraasilimia58% ikifuatiwa Mara55%.
Aidha ameongeza Takwimu za Mwaka 2010 za DHS zinaonesha katika kanda ya ziwa Mara iko
chini sana kwa matumizi ya uzazi wa mpango kwani
asilimia9.8 tu wanawakeutumia uzazi huo wa mpango.
Hata hivyo mkoa wa mara kwa takwimu za mwaka 2010 asilimia
72% inaongoza katika vitendo vya ukatili wa kimwili na kijinsia ikifuatwa
Dodomaasilimia 71, na ya tatu pemba asilimia 05,
Sanjari na hayo imeonekana kuwa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 haiwalindi watoto watoto wa
kike wenye umri chini ya miaka18dhidi ya kuolewa bali sheria hiyoinaruhusu
wasichana wenye umri wa miaka 14 kuolewa kwa ridhaa maalum na mara nyingi
uruhusu wasichana wa miaka 15 kuolew kwa ridhaa ya wazazi wao hali ambayo
inazidi kuathili maendeleo ya motto wa kike.
Hivyo mkurugenzi huyo alisema kuwa serikali haina budi
kurekebisha sheria hiyo ili kuwalinda watoto wa kike.