TGNP yaungana na wananchi kupinga ukatili kuanzia kesho Wilayani Traime



TGNP yaungana na wananchi kupinga ukatili kuanzia kesho Wilayani Tarime

TGNP MTANDAO usikuwa wa kiserikali  kesho weanatarajia  kufanya tamasha katika viwanja vya shule ya msingi
N'geren'gere kata ya Nyamaraga wilaya ya Tarime mkoani  Mara, kwa kupinga
ukeketaji wa watoto wa kike wa shule za msingi na sekondari.

Tamasha hilo litapinga ukatili wa kijinsia katika ndoa za utotoni kwa
wanafunzi wa shule hizo na ukosaji wa hali za umilki wa rasilimali Adhi
katika ngazi ya familia.

Ofisa  Habari wa TGNP MTANDAO Deogratias Tembo aliwaambia waandishi wa
Habari mjini hapa kuwa mgeni rasimi wa tamasha hilo  ni mkuu wa wilayani
hapa John Henjewele.

Temba alisema kuwa tamasha hilo limekuja baada ya kupata takwimu za ndoa za
utotoni, ukeketaji na unyanyasaji wa kijinsia kuondelea kuongezeka katika
wilaya ya Tarime vinavyotokana na kuendekeza mfumo dume.

Alisema walifikia hatua hiyo kuitaka jamii iachane na kukumbatia mila na
desturi zinazochangia kiasi kikubwa katika jamii kukumbatia mfumo huo.

'' Lengo la kuleta tamasha hili wilaya ya Tarime ni kutokana na kuitaka
jamii ibadilike na kuingia kwenye mabadiliko kwani wilaya ya Tarime, ni
miongoni mwa wilaya nchini jamii yake kuendekeza ndoa za utotoni, ukeketaji
kwa watoto wa kike wa shule za msingi na sekondari na kuwakwamisha kufikia
malengo ya ndoto zao'' alisema Temba.

Alisema kuwa wanyeji wa tamasha hilo ni kituo cha Taarifa na maarifa cha
kata ya Nyamaraga ambalo litachukua siku tatu kuanzia kesho, liliandaliwa
na TGNP MTANDAO kwa kushirikiana na shirika la kibinafsi la ACTION AID.

Washiriki na walengwa na  tamasha hilo alisema kuwa wazee wa kimila wa koo
zote 13 za kabila la wakurya pamoja na Jeshi la Polisi kupitia dawati lao
la jinsia.

Wengine aliwataja Temba kuwa ni pamoja na viongozi wengine wa Halmashauri,
maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii na wale wa idara za Afya, Kilimo,
maji na jamii.

Powered by Blogger.