Waandishi wa habari watakiwa kuandika habari zenye ukweli
Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA Bi: Valeria Msoka akiongea na waandishi wa habari katika semina inayoendelea jijini Mwanza kwenye ukumbi wa Midlkand Hotel kwa lengo la kuzungumzia vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya mama na mtoto kulia kwake ni mkurugenzi wa UTPC Bw:Abubakar Karsan
Mwanza
Mwanza
Waandishi wa habari wametakiwa kuandika habari za kweli na
si kuandika habari zenye uchochezi ambao unaweza kuvuruga amani ya Tanzania
Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi mtendaji wa UTPC
Bw:Abubakar Karsan katika ufunguzi wa mafunzo ya waandishi wa habari
kutoka katika mikoa mitano ya kanda ya
ziwa yaliyoandaliwa na chama cha
waandiishi wa habari wanawake Tamwa na kufadhiliwa na (UNFPA) yanayo
fanyika katika ukumbi wa Midland hoteli jijini Mwanza kwa takribai siku tatu.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa waandishi wa habari wasimamie ukweli kwa lengo la kubadilisha
jamii na si kukalia kuandika habari za kiuchochezi zenye maslahi ya watu
binafsi.
“Tumieni vizuri fursa mnazozipata kwa lengo la kubadili
jamii inayowazunguka pia waandishi ondokana na suala la kulazimisha posho”
alisema Mkurugenzi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari
Varelia Msoka alisema kuwa waandishi wa habari waendelee kuibua mambo ambao
yamejificha lengo la kuleta mabadiliko.
“Kupitia TAMWA tunazidi kupambana kwa kushirikiana na Mashirika mengine lakini bila nguvu ya waandishi wa habari ujumbe tuliokusudia
hautafika maeneo huska” alisema Msoka.
Hata hivyo mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Mafunzo hayo
ambayo yatakuwa takribani siku tatu kwa waandishi wa habari kutoka Mikoa ya
Mwanza, Shinyanga, Kagera,Mara na Simiyu kwa lengo la kupata mafunzo juu ya
kuandika habari za ukatili wa kijinsia dhidi
ya mama na mtoto.
Aidha mkurugenzi huyo alisema kuwa waandishi hao wasimamamie
ukweli na kuibua vitendo vya ukatili ambavyo vimeshamiri ususani mikoa ya
Shinyanga, Simiyu na Mara ili kuweza kuleta mabadiliko.
Washiriki wa mafunzo hayo walisema kuwa watakuwa mstali wa
mbele kwa lengo la kuzidi kuibua changamoto zilizopo vijijini ili kuleta
mabadiliko.