Nyambari akemea siasa Mashuleni:
Nyambari akemea siasa
Mashuleni:
Mbunge wa jimbo la Tarime Nyambari Nyangwine amekemea sula
la siasa mashuleni kwa lengo la kunusuru wanafunzi ili kuongeza ufahuru wao.
Kauli hiyo ilitolewa jana kipindi akiongea na vyombo vya
habari kuwa baadhi ya walimu na
wanafunzi wamekuwa wakiendesha suala zima la siasa shuleni .
Nyambari alisema kuwa baadhi ya walimu wamekuwa kichocheo
kikubwa cha kuanzisha suala zima la siasa mashuleni na kupelekea wanafunzi kufeli masomo kwani walimu hao utumia muda mwingi kujadili mambo ya
siasa na kupoteza muda wa kufundisha masomo yao.
Natoa mwito kwa walimu wote kuondokana mara ,moja na mambo ya kisiasa mashuleni pia walimu wawe
wakali kwa ajili ya kuwakanya wanafunzi ambao wanajiingiza katika masuala ya
kisiasa na mwisho wake kufeli masomo alisema
Nyambari.
Aidha mbunge huyo aliongelea suala zima la njaa ambalo
limekumba baadhi ya kata na kusema kuwa watendaji wa vijiji wawe wazi katika
kutoa taarifa sahii ili kuwa na takwimu nzuri za kubaini familia zilizokumbwa
na njaa ili ziwezekupata msaada wa chakula mara moja.
“Watendaji hawatoi takwimu sahii ili tipate familia sahii
zenye mahitaji suala ambalo ni changamoto kwetu”alisema mbunge.
Hata hivyo mbunge huyo wa jimbo la Tarime amekemea vitendo
vya jeshi la polisi amabavyo vinatendeka ususani kunyanyasa raia, kubandikia
kesi waondokane navya mara moja.
“Mtu yeyote
anayenyanyasa masikini lazima nipambane naye kila raia anahaki ya kupata huduma
nzuri na si kunyanyaswa tunataka Tarime byenye Amani, Upendo. Ushirikiano
pamoja na Mshikamano” alisema Nyambari.
Mwisho mbunge amekemea baadhi ya watu ambao wameanza kampeni
zao mapema wasije wakasababisha uvunjifu wa amani pia waondokane na kutumia
vibaya vijana kwa ajili ya uchochezi wa vujo.