Diwani wa kata ya Ikoma ahamasisha michezo
Diwani wa kata ya Ikoma wilayani Rorya mkoani Mara Laurent Adriano amehamasisha
suala la michezo wilayani humo kwa lengo la kuwabadilisha mitazamo hasi vijana
waliyonayo.
Diwani huyo alisema kuwa suala la michezo ni ajira hivyo
vijana hao hawanabudi kulitililia mkazo kwa lengo la kujiaji;li wenyewe na si
kusubili kaujiliwa na serikali ikiwa ni pamoja na kudumisha Upendo, Amani
pamoja na ujirani mwema baina ya kata jirani kupitia michezo hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na diwani hiyo katika kukabidhi
zawadi za kombe la Adrian Cup 2014-2015 lililokuwalikishindaniwa katika
uwanja wa kogaja huku timu kumi na moja kutoka katika vijiji vitatu
vilivyomo ndani ya kata ya ikoma wilayani Rorya zikishiriki mashindano hayo,
“Lengo langu la kuanzisha mashindano haya ni kuhamasisha
vijana kupenda michezo hivyo naomba mudumishe michezo na tusiishie hapa tuweza
kupata timu mbili na kushiriki ngazi ya mkoa hadi Taifa” alisema Diwani.
Katika michuano hiyo Timu ya Young Stars iliibuka kidedea
baada ya kuichapa timu ya Lwanda fc kibao cha 1-0 ambapo bao lilifungwa na
George Bededict dakika ya 15 kipindi cha kwanza ambapo iliweza kudumu mpaka
dakika za mwisho.
Mshindi wa kwanza mpaka wa tano waliweza kupata zawadi
mbalimbali amabapo mshindi wa kwanza alipewa shilingi laki nne na elfu
themanini na seti moja ya jenzi, mshindi wa pili laki tatu na elfu themanini,
mshindi wa tatu laki mbili na elfu
themanini, mshindi wa nne laki moja na elfu themanini na mshindi wa tano
alipwewa shilingi laki mija na elfu thelathini huku kuanzia mshindi wa sita
mpaka timu ya kumi na moja ikipewa zawadi ya shilingi elfu themanini kwa kila
timu.
Katika fainali hiyo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa chuo cha
uhasibu kilichopo Arusha Prof Johannes Monyo ambapo alihaidi kwa kila timu
kutoa seti ya jenzi ili kuweza kudumisha michezo wilayani humo.
“Nimetoka mbali kuja kushudia michuano ya Adrian Cup
2014-2015 kwa lengo la kuwapa vijana moyo ili wapende mochezo kwani michezo ni
ajira tumieni fursa hizo za michezo vizuri na msibadilishwe na wachache wenye
nia yao
binafsi” alisema Profesa Monyo.
Hata hivyo mgeni rasmi huyo alimwomba diwani huyo kutoishia
hapo bali vijana waendelezwe katika suala zima la michezo huku wakitafutiwa
wafadhili
…….Mwisho….