Vijana wanaozunguka mgodi wa Barrick wapewa mafunzo ya ujasiliamali:
Nick wa pili akitoa mada kwa vijana kutoka vijiji saba vinavyozunguka mgodi wa dhahabu wa Nyamongo wilayani Tarime Mkoani Mara katika semina ya mafunzo ya ujasiliamali na kujua utumiaji wa fursa walizonazo
Vijana zaidi ya miambili kutoka katika vijiji saba vinavyozunguka mgodi wa dhahabu wa Norht
Mara wa African Barrick Gold Mine (ABG)
uliopo Nyamongo wilayani Tarime Mkoani Mara wamepata mafunzo ya utumiaji wa fursa zilizopo kwa lengo la
kujikomboa kiuchumi.
Mafunzo hayo yameanza Julai 4 na kuitimishwa Julai 5 Mwaka
huu katika shule ya sekondari Ingwe huku
yakidhaminiwa na Mgodi wa North Mara pamoja na Clouds Media
Group ili vijana waweze kutambua umuhimu wa fursa zilizopo kwa lengo la
kuwanufaisha kimaisha.
Katika mafunzo hayo zimekuwa zimejadiliwa mada kama vile jinsi ya kufanya ujasiliamali wenye tija, Elimu
juu ya matumizi ya fedha,Elimu ya Afya,Nidhamu ya Mafanikio uwapo kazini, Namna
ya kubuni na kuzitambua kwa manufaa ya
kuzitumia katika kuboresha maisha , Na jinsi ya kupata masoko na kuyatumia.
Aidha vijana hao katika kuwasilisha mada wameuomba mgodi huo
kuwapa maeneo ya uchimbaji mdogo kwa lengo la kujipatia kipato na kusema kuwa
mafunzo hayo yamewafumbua macho kwa sasa.
“Tumekuwa tukishindwaz kutumia vizuri fursa zetu na
rasilimali tulizonazo kwa kukosa elimu tuliyoipata nadhani tutafanya mapinduzi”
walisema washiriki hao.
Katika kutoa mafunzo hayo Msanii maarufu wa mziki wa hip hop
Nick wapili amewataka vijana hao kulipa
kipaumbele suala la Elimu ili waweze kuijikomboa wao na kuwataka vijana hao
kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa lengo la kunufaika
“Mitandao ya kijamii ukiitumia vizuri nfano katika kusoma
unaweza kunufaika lakini vijana waliowengi mnatumia mitandao hiyo tofauti suala ambalo
limewakumba vijana wengi na kupoteza mwerekeo wa maisha” alisema Nick wa pili.
Budeki John kutoka katika kijiji cha Nyangoto alisema kuwa
fursa hiyo ya kupata mafunzo hayo kwao imekuwa bahati kubwa hivyo amewataka
vijana wenzake kutambua fursa hizo na kuzitumia vizuri kwa lengo la kunufaika kimaisha na kubadili
mitazamo waliyonayo ya kuvamia mgodi huo mara kwa mara ili kupata mawe ya
dhahabu.
“Vijana tuvamia mgodi na kupata fedha nyingi lakini
tunazitumia vibaya kupitia elimu tuliyoipata vijana watabadilika” alisema
Budeki.
Nikodemus Keryaro ni ofisa ushirikishwaji alizitaja changamoto zinazokumba jamii inayozunguka
mgodi huo kuwa hawako tayari kutumia vizuri fursa hizo wanazozipata kwa lengo
la kubadilika na kuongeza uchumi.
“Tulitegemea kupata vijana zaidi ya miasita kutoka vijiji
saba vya mgodi lakini idadi iliyopo ni chache na wengine wapo darasani lakini
hawazingatii masomo hayo na ni wachache watakao yafanyia kazi” alisema
Nicodemus.
Kwa upande wake ofisa maendeleo ya jamii kutoka African
Barrick Gold Mine (ABG) North Mara BeatriceThobias aliitaka jamii kutumia
ipasavyo fursa kama hizo kwani fursa hizo zimefika
maeneo ya vijini na kuongeza kuwa fursa hizo zimeanza kufika maeneo ya vijijini
hivyo jamii iondikane na dhana potofu ambayo imejijengea kwa lengo la kuleta
mabadiliko.
“Fursa hizi zimekuwa zikitoka maeneo ya mjini na jamii
inachangila lakini hapa jamii inapata
mafunzo bure kupitia Mgodi huu na Cluds Media Group bado mwitikio ni
mdogo sana
inabidi jamii kubadilika na kuchangamkia fursa hizi mara moja” alisema
Beatrice.