Mashirika elekezeni nguvu kubwa vijijini:
Mashirika elekezeni
nguvu kubwa vijijini:
MAKALA:
Mashirika mbalimbali yamekuwa mstari wa mbele kwa lengo la
kutokomeza suala zima la ukatiki wa kijinsia ambao umekuwa tishio katika mikoa
mbalimbali dhidi ya mama na motto.
Katika tamasha la kupinga
ukatili wa kijinsia dhidi ya akinamama na mtoto lililofanyika hivi karibuni katika shule ya msingi Ng’ereng’ere kata Nyamaraga Wilayani
Tarime mkoani Mara imebainika kuwa mkoa
wa Mara unaongoza kwa ukatili wa kimwili dhidi ya mtoto wa kike kwa asilimia72 ukifuatiwa na mkoa wa Dodoma wenye
asilimia71 na mkoa wa Pemba wenye asilimia
05 huku mashirika yakizidi kupambana na suala hilo kwa lengo la
kumkomboa mtoto wa kike.
TGNP Mtandao umeweza kubainisha takwimu hizo za mwaka 2010 katika
tamasha lililoandaliwa likichukuwa takribani
siku tatu huku mada mbalimbali zikiongelewa kwa lengo la kufikisha ujumbe katika jamii.
Kongamano,Mbalimbali za kupinga ukatili huo zimekuwa zikifanyika
maeneo ya mjini na si vijijini wakati waanga wakubwa wako maeneo ya vijijini
suala amabalo bado ni changamoto kwa mashirika hayo lakini kwa kutambua umuhimu
wa mtoto wa kike mashirika hayo yameweza kuunganisha nguvu za pamoja na kufika
maeneo ya vijijini kwa lengo la klutoa
semina na mafunzo mbalimnbali juu ya kupinga ukatili dhidi ya mamana mtoto,
Ndoa za utotoni, ukeketaji pamoja na Mimba za utotoni.
Tumekuwa tukiona juhudi za chama cha waandishi wa habari
wanawake (Tamwa) kupitia mkurugenzi wake Varelia Msoka wakiunganisha nguvu ya
pamoja kwa lengo la kumlinda mtoto wa kike pale anaponyimwa haki yake,
anaponyanyaswa aidha kingono, kiakili mashirika hayo uinesha juhudi za makusudi
kwa lengo la kuleta mabadiliko katika sehemu
husika.
Hata hivyo chama cha waandishi wa habari wanawake(TAMWA)kimekuwa pia na juhudi za kutoa
mafunzo mbalimbali kwa waandishi wa
habari ili kuwajengea uwezo na uelewa pamoja na ujasili wa kuendelea
kuandika vitendo vya ukatili ili jamii kuweza kubadili mienemndo na mitazamo
waliojijengea.
Juhudi hizo za
mashirika mbalimbali, CBO,NGOS, CSO zimeweza kusaidia kupunguza vitendo hivi
vya ukatili kwa kiasi fulani japo waanga wengine hawajafikiwa kulingana na
mazingira waliyopo hivyo serikali kwa kuunganisha nguvu za pamoja hawana budi
kufika maeneo ya vijijini ili kuokomesha vitendo hivyo vya kikatili.
Kwa upande mwaingine vitendo hivi nanaonekana kukua kwa kasi
ni baada ya jamii kupata elimu za kutosha na kuanza kutoa taarifa kwa vyombo
husika na kufanyiwa kazi kwani awali vitendo hivyo vilikuwa vikitendeka na
jamii inakaa kimya.
Ndoa za utotoni,Mkoa
wa Marani kati ya mikoa mitatu nchini
Tanzania ambayo inaongoza kwa kiwango kikubwa saa cha ndoa za utotoni takwimu
za kitaifa zinaonesha zaidi ya nusu ya
wasichanae wadogo wanaozeshwa mikoa minginea ni pamoja na Shinyanga
asilimia59% Tabora58% ikifuatiwa Mara asilimia55% na uku utafiti ukionesha mkoa wenye asilimia
ndogo katika suala zima la ndoa za utotoni Iringa 08%.
Merry msemwa ni meneja wa
programu katika uanarakati,
Utafiti na Ushawishi pamoja na Utetezi katika TGNP Mtandao katika tamasha hilo
alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa tamasha hilo ambalo litachukua takiribani
siku tatu nikuweka mikakati mahususi ili kila mtu kuweza kupata fursa ya
kushiriki tamasha hilo na kutoa mawazo yake.
“Matamasha haya tumekuwa tukiyafanyia Dar –es salaam lakini
mwaka huu tumeamua kufika kwa walengwawenyewe wanaokumbwa na masula ya ukatili
wa kijinsia” alisema Mery.
Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za
wanawake la kivulinilililo po jijini
mwanzaBi: Maimuna Kanyamala katika kutoa
mada halisi juu yua ukeketaji na ndoa za utotoni mbele ya mgeni rasmi Ofisa Tawala wa wiliya
Baraka Nyamsenda kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Tarime John Henjewele alisema
kuwa wameamua kuongelea mada hiyo kwa sababu wanajali utu wa jamii nzima bila
kujali umri, elimu,dini,na itikadi ya
vyama.
Mgeni rasmi huyo alitoa mwito ka jamii kuwa waweze kufichua
jamii ambayo inazidi kukumbatia vitendo hivyo vya kinyama kwa lengo la kupunguza ukatili huo ndani ya wilaya ya
Tarime.
“Siri mnazotunza kwa
watu wanaotenda unyama huo ndo
changamoto kwa mashirika Halmashauri kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya
tupo bega kwa bega kupinga vitendo hivyo toeni taarifa vyombo vya sheria viko
wazi” alisema mgeni rasmi.
Hta hivyo Mkoa wa
Mara kwa kanda ya ziwa takwimu za mwaka2010 za DHS zilionesha kuwa Mara iko
chini sana kwa matumizi ya uzazi wa mpango kwani ni
asilimia 9.8 ya wanawake wanaotumia uzazi wa mpango hali ambayo imeongeza nguvu
kubwa ya kuweza kuelimisha wanawake kuhusu huduma hiyo.
Changamoto,pamojana
kwamba ndoa za utotoni zina athali kubwa sana
pamoja na kupoteza maisha ya watoto wa kike, sheria ya Ndoa ya mwaka
1971haiwalindi wasichana wenye umri wa miaka18 dhidi ya kuolewa, kwani sheri
hiyo uwagusa wasichana wenye umri wa miak14 kuolew kwa ridhaa maalumu na
maranyingi inaruhusu wasichana wenye umri wa miaka 15 kuolewa kwa ridhaa ya
wazazi wao, Hali hii inaathiri maendeleo ya wasichanahisikana taifa kwa ujumla
wanaharakati wa masuala ya kijinsia na
haki zabinadamuwamejitaidi kwa muda mrefu ili iweze kufanyiwa marekebisha bila
mafanikio.
Ukeketaji,Pamoja
na kuwepo kwa juhudi mbalimbali za kusitisha ukeketaji ikiwepo sheria
inayozuia, hali halisi ya ukeketaji kwa watoto wa kike bado ni mbaya mkoa wa
Mara kati ya mikoa 5 ya kitanzania ambayo inaongoza katika ukeketaji, Takwimu
za afya za Taifa za mwaka 2010 zimedhihirisha kwamba asiloimia39 ya
wanawakewamekeketwa.
Ukeketaji huo unaofanyika katika mikoa mbalimbali hapa
Tanzainia ikijumuishaMara imechangia wanawake million tatu ambaoni sawana asilimia14.6
ya wanawakeawote nchini wote wamekeketwa.
Mwaka 2004 hali halisi ya ukeketaji mkoani Mara ilikuwa
asilimia38.1 hatahivyo kufikia mwaka 2010 vitendo hivyo vimeongezeka hadi
asilimia 39.9amabalo ni angezeko la asilimia1.8,ongezeko hilo linaonesha kuawa
badojuhudi za serikali na mashirika kwa kushirikiana na jamii bado nindogo
sana.
Toka kuanzishwa kwa TGNP Mtandao mwaka1993 wamekuwa mstari
wa mbele katika kupigania haki na usawa wa motto wa kike ikiwa ni pamoja
nakupinga vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji,
BadoTanzaniakumekuwepo na changamoto kubwa kwa vituo vya
polisi na idara za ustawi wa jamii kutokuwa na mahala salama pa kuwahifadhi
wahanga wa ukeketaji na hiyo kusababisha wasichana wengi ambao wameelimishwa na
kuelewa madhara ya ukeketaji kujiluta
wanaburuzwa kwa nguvu kupitaia vitendo
hivyo.