Asakwa kwa kubaka:
Asakwa kwa kubaka:
SIKU mbili baada ya Shirika
la TGNP kuandaa tamasha la kupinga vitendo vya ukati,unyanyasaji,ndoa za
utotoni na ukeketaji kwa watoto wakike vinavyo fanywa na baadhi ya watu
wenyeuelewa mdogo Wilayani Tarime Mkoani Mara Binti wa Miaka kumi amedaiwa
kubakwa na kuumizwa vibaya katika viungo
vyake na Kijana wa miaka 23.
Akielezea tukio hilo Afisa Mtendaji wa
Kijiji cha Motana Amosi Sameli alisema kuwa walikuwa katika kikao cha Katibu
Tarafa Inano Marwa Lutha Ofisini kwake majira ya saa 6_7 mchana tarehe,03,07,2014
ambapo gafla walisikia yowe ikipigwa walipotaharuki walikuta watu wengi wakiwa
wameandamana wakiwa na Binti huku wakisema kuwa amekimbia mbakaji.
‘’Nilipo sikia kelele hizo
ilinibidi nifuatilia kwa karibu ambapo kundi hilo la watu waliniambaia kuwa wamemkuta
binti huyo akiwa anagaragazwa chini na kijana Nyitika Wiliphabosi 23 wa
kijijini hapo kwa lengo la kutaka kumbaka ambapo kijana huyo amefanikiwa
kutoroka baada ya watu kuwa wamefika
katika eneo la tukio’’alisema Samweli.
Samweli aliongeza kuwa alitoa
ushauri kwa wazazi wake kwenda kutoa
taarifa kituoni polisi na kupewa PF3 kwa ajili ya kwenda hospitali kupata
matibabu ambapo mzazi wa kike wa binti
huyo Mery Marwa Lutter 50 alifuata ushauri huo na kuchukua hatua ya kumpeleka
kituoni polisi na kupata PF3.
Akitoa
maelezo mbele ya mwaandishi wa habari hizi Mamam mzazi Mery wa binti huyo
ambaye jina tunalihifadhi alisema kuwa Mbakaji alimdanganyishia kwenda kumpa
nyama kwa ajili Mtoto kwa lengo la kwenda kupika katika Mgahawa Mama ntilie kijijini hapo
ambapo alifika njiani na kuanza kumlazimisha kuvua nguo ambapo binti huyo
alikataa na kuanza kulia huku
akipiga yowe ambapo nilisikia na kutuka nje kijana huyo alipo ona
hivyo alimwaacha na kuzunguka upande wa pili kumvizia tena njiani.
‘’Mara
yapili alimfutaa tena akiwa anarudi kipandani kwa mamantilie ambapo alimkaba na
kumchukua kinguvunguvu huku akiwa anamtishia hadi vichakani mbali kidogo na
Nyumbani kama mita 300 ambapo aliazna kumvua nguo na kuanza kushiriki naye kwa
nguvu kumlazimisha kuchukua hela ili asiseme ambapo nilisikia keleke nikatoka
nikafuata zinakotokea ni kakuta ni binti yangu akiwa anabakwa na yuleyule
kijana kwa mara ya pili’’aliongeza kusema Mama huyo.
Kwa
upande wa Msaidizi wa kisheria kituo
cha manga Ayubu Gabriel alisema kuwa amesikitishwa na kitendo hicho na kuomba
Serikali kutoa makucha kwa wale wote ambao wanabainika kufanya vitendo kama hivyo.
Aidha
Gabriel alitoa rai kwa jeshi la polisi kuhakikisha kuwa mtuhumiwa wa tukio hilo anakamatwa na kufikishwa katika sehemu husika
na sheria kuchukua mkondon wake.
Tamwa
ni chama cha waandishi wa habari wanawake wamekuwa mstari wa mbele kutetea haki
za binadamu naye Mkurugenzi wa chama hicho Varelia Msoka alipopigiwa simu
kuhusiana na tukio hilo
alisema kuwa jamii isimamie ukweli na iweze
kujitokeza
mahakamani kwa lengo la kupata haki zao za msingi.
Jamii
ijijengee msimamamo wa kusimamia ukweli ilikuweza kutokomeza vitendo hivi vya
kinyama alisema Bi:Msoka
Hata hivyo Bi Msoka amekeamea kitendo hicho cha
kinyama na kutoa wito kwa jamii kuondokana na vitendo vya kinyama kwani vitendo
hivyo vinawanyima watoto haki zao za msingi.
……..Mwisho…