VIKOBA OMBENI MIKOPO BENKI:
Asasi za kuweka na kukopa (VICOBA
) zimeshauriwa kukopa mikopo katika banki mbalimbali kwa lengo la kutunisha
mifuko yao ili
kuweza kuendeleza miradi mbalimbali
waliyonayo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwakilishi
wa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Tarime Venance Mwamengo katika kujibu taarifa ya utendaji kazi wa kikindi
cha kuweka na kukopa Tujijenge VICOBA
katika ukumbi wa Bwaro la polisi Wilayani Tarime Mkoani Mara.
Mgeni rasmi huyo Bw:Pedas Masungwa
kwa niaba ya mkurugenzi wa mji wa Tarime
alisema kuwaVicoba hivyo viweze kutuma Maandiko mbalimbali katika
Taasisi kubwa za kifedha kwa lengo la kupata mikopo na kuweza kutunisha mifuko
yao ili kuweza kukopesha wanachama hao fedha za kutosha.
“Tunazo taasisi nyingi za kifedha
NMB, CRDB tumeni andiko ili muweze kukopeshwa fedha za kutosha kwa lengo la
kupanua miradi mliyonayo pia wekeni miradi yenu
sehemu zenye ushindani mkubwa”
alisema mgeni rasmi.
Mkufunzi wa VICOBA hivyo Bw : Emmanuel Buchafwe katika kuwasilisha taarifa ya VICOBA kuanzia
04 julai Mawaka jana mpaka 29 juni Mwaka huu
alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa asasi hiyo kuinua hali ya maisha kwa wanachama na familia zao
kijamii, kiuchumi,kimazingira na kitamaduni ambapo kwa sasa tangu kuanza ni
miaka mitano, kikundi kwa sasa kina
wanachama 30 wanawake 26 na wanaume 4 na walianza wakiwa wanachama 17 ongezeko
la wanachama 17.
Hata hivyo mkufunzi huyo aliyataja
mafanikio ya kikundi hicho kuwa wanacha wameweza kusomesha watoto, kuendeleza
bihashara zao,kusaidia maafayanapotokea,wanachama kutumia rasilimali muda na
fedha kwa kubuni na kuanzisha mradi wa mashine tatu mashine 2 za kusaga na 1 ya
kukoboa ukiwa na thamani ya shilingi 8,3000,000fedha za kitanzania
Sanjari na hayo alizitaja
changamotozinazowakabili kuwa ni Wanachama kutorejesha mikopo kwa
wakati,kutozingatia katiba ya kikundi hicho,jamii kutojua umuhimu wa mfano
jinsi unavyosaidia jamii yenye kipatocha chini,na wanachama kutoweka staid za
maarifa,mbinukatika kusimamia miradi ya kiuchumi.
Wameitaja mikakati waliyonayo kuongeza miradi ya
kiuchumitoka asilimia30%ya sasa hadi kufikia asilimia 60%, kuboresha ukopeshaji
wa kwa kupunguza nyongeza na bimatoka asilimia15%ya2013 hadi asilimia10 ya
2014-2015 pamoja na kununua kwa mashine yenye uwezo wa kusaga,
kukoboa,kupimakupakia na kushona mifuko uku wakitoa changizo la shilingi kwa
lengo la kutunisha mifuko yao.
Wanachama hao wa Tujijenge VICOBA
wameomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Tarime kuwapa eneo kwa lengo la
kujenga ofisi zao ili kuweza kufanyakazi kwa ufanisi.
……….Mwisho…….