Nusuru shilingi elfu mbili imutoe roho binti mwenye umri wa miaka 18 wilayani Tarime mkoani Mara;
Nusuru shilingi elfu
mbili imutoe roho,
Binti mmoja aliyefaamika kwa jina la Agness Marwa Chacha mwenye umri wa miaka 18 mkazi wa
kijiji cha Murito kata ya kemambo(Nyamongo) wilayani Tarime mkoani
Maraamenusurika kuawa na mme wake
aliyefaamoka kwa jina la Marwa chacha
kisyengi mkazi wa mrito mkulima.
Binti huyo alichomwa vikali sehemu za siri kwa kiginga cha
moto na makalio yake na mmewe kwa kile kinachosemekana ni wivu wa kimapenzi ni
baada ya mme wake binti kukuta shilingi elfu mbili katika pochi na kuanza
kumushambulia kwa fimbo.
“Alipo fika nyumbani alinikuta na kuniuliza kuwa pesa
iliyokuwa kwenye pochi imetoka wapi nakudai kuwa nimeongwa na wanaume wakati
hiyopesa nilikuwa siijui ndipoa aliaanza kunipiga baadae kaniweka njee
akanifunga nikanyeshewa mvua badae akatafuta kiginga cha mota akaanza kunichoma
sehemu zangu za siri na makalio” alisema Agness.
Mganga mkuu katika hospitali ya sungu sungu Dr kagumilwa
kaijage ambapo alilazwa mgonjwa huyo alisema kuwa binti huyo baada ya
kuungunguza julai 13 mwaka huu hakuweza kuripoti hospitalini na badala
yake ariripoti julai 17 mwaka huu na kuanza kuripotiwa akiwa
ameaoaza sehemu za siri na mapaja.
“Tumempokea haspitali akiwa ameisha oza sehemu zake za siri
zikitoa usaha na kuanza kutoa huduma”
alisema mganga mkuu.
Kwa mjibu wa maelezo ya docta binti huyo mbali na kufanyiwa
vitendo hivyo vya ukatili ana mimba ya mwezi mmoja na nusu.
Kupitia mashirika mbali mbali ya kutetea haki za binadanu
likiwemo chama cha waandishi wanawake Tamwa chini ya mkurugenzi wake
varelie msoka wamekuwa mstari wa mbele kupigania haki ya
mwanamke ikiwa ni pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia lakini
jamii haiku tayari kubadilika.
Kulingana na nukuu iliandaliwa na chama hicho cha waandishi
wa habari wanawake Tamwa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kama
ilivyofanyiwa marekebisho ya mwaka 1977 na mwaka 2001 inatambua haki ya kila
binadamu sasa inakuwaje jamii inakiuka sheria hii na serikali inakaa kimya japo
mashirika yasiykuwa ya kiserikali yanazidi kulipigania kwa lengo la kureta
mabadiliko na kama ilivyo ibara ya
13:6(e) ya katiba inayosema ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa, kinyama au
kupewa adhabu ya kudhalilishwa lakini vitendo hivi vimekuwa vikiendelea na
serikali imekaa kimya.
Kwa upande wake mama mazazi wa binti huyo Bi Nsato Marwa alikemea vikali kitendo hicho
cha kinyama na kuiomba serikali kulivalia njuga ili mtuhumiwa kutiwa hatiani
kwa ili liwe fundisho kwa jamii.
“Mwanangu ameharibiwa na mimi sina pesa za kumfanyia
matibabu naomba msaada kwa Taasisi za serikali na zisizokuwa za kiserikali
mashirika ili kuweza kunusuru mwanangu walikuwa wakimsaidia katitika matibabu
wametoroka baada ya kusikia wanatafuitwa na jeshi la polisi” alisema mama mzazi.
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Tarime Rorya kamishina msaidizi wa polisi Lazaro Benedict alidhibitisha
kutokea kwa tukio hilo
la kinyama na kusema kuwa na kuwataka jamii hiendelee kutoa taarifa mapema
kwani taarifa hizo walizipata wakiwa wamechelewa.
………Mwisho….