KAMPUNI ZA KUNUNUA TUMBAKU ZAOMBWA KUJA KUWEKEZA TARI
KAMPUNI ZA KUNUNUA TUMBAKU ZAOMBWA
KUJA KUWEKEZA TARI
Tarime:
WADAU wa Tumbaku
Wilayani Tarime Mkoani Mara wameomba makampuni mbalimbali yanayo nunua zao la
tumbaku kujitokeza kuja kuwekeza Tarime ili kuwepo na ushindani wa bei ya
kununulia badala ya kampuni ya ALLANCE ONE iliyopo.
Wadau hao walisema hayo
juzi,24,2014 Kwenye semina ya kuwajengea uwezo wadau wa tumbaku iliandaliwa na
Taasisi ya Utafiti wa Tumbaku Tanzania (TORITA) juu ya Uandaaji na utunzaji
sahihi wa vitalu(uwekaji wa pepete na mbolea).
Akizungumza Veronika
Gabriel ambaye ni Ofisa Tumbaku wilayani Tarime kwa niaba ya wenzake alisema
kuwa wakulima wa zao la tumbaku Wilayani Tarime wanapunjika wakati wa kuuza
tumbaku kwa kampuni ya Allance One kuwa moja na kuwa kampuni hiyo haina
mshindani hali ambayo inasababisha wananunua zao hilo kwa kujisikia.
''Kampuni ya Allance One
unanunua Tumbaku kutoka kwa wakulima kwa kujisikia ambapo kwa kilo moja ya
tumbaku watoa Tsh 350,badaya ya Tsh 3500 ambayo Kampuni ya Allance One ya Kenya
inanunua kutoka kwa wakulima wakati wanapo peleka kuuza huko''alisema Veronika.
Aidha Veronika aliongeza
kuwa kutokana ukosefu wa soko la uhakika wakulima wa Tumbaku wametishia kuchoma
tumbaku likiwa shambani na kupanda mazao mengine ili kuondokana na usumbufu
wanaoupata na pia kutorosha tumbaku kwenda Nchi jirani ya Kenya kunasababisha
halmashauri kukoswa mapatoaliongeza kusema.
Kwa upande wake Afisa
Mafunzo ambaye ametoka taasisi ya utafiti wa Tumbaku Cleophace
Mathias alisema kuwa jukumu la kampuni iliyo kubaliwa kununua tumbaku kisheria
inatakiwa kufuata taratibu zilizopo pasipo kuzikiuka.
Aidha Mathias aliongeza
kuwa uongozi wa Serikali unapaswa kusimamia taratibu zilizowekwa ili kuwasaidia
wananchi wake na kuhakikisha kuwa makampuni yanalipa ushuru na pato la Taifa
linaongeze na Wananchi wake wananufaika.
,,,,,mwisho…