Jamii yatakiwa kudumisha upendo,Amani na Mshikamano:
Jamii yatakiwa kudumisha upendo,Amani na Mshikamano:
Tarime:
KANISA la Wadiventista
Wasabato Mara Conference la Tarime kati limewataka waumini wa kanisa hilo
kufanya kazi ya Uinjilisti na kudumisha upendo kwa lengo la kuongoa Roho
za Watu kwenda kwa Y esu ambao wanapotea bila kumjua mwenyezi Mungu.
Kauli hiyo imetolewa na
Mzee wa kanisa hilo Alphonce Maigga jana wakati akihutubia Washiriki katika
ibada ya kuhamasisha siku ya changizo la harambee ambayo inatarajiwa
kufanyika hapo September,09,2014 kwa ajili ya upanuzi na Ujenzi wa kanisa ili
kukidhi mahitaji ya Kanisa.
Maigga alisema kuwa
Kanisa ni chombo ambacho kiliundwa na Mungu mwenyewe kwa lengo la kumwakilisha
hapa Duniani na kuwa kufanya kazi ya uijnjilisti ni kufanya moja ya kazi
ambazo Bwana Yesu aliifanya hapa Duniani.
Aidha Maigga aliongeza
kusema kuwa kazi ya Uinjilisti ni moja ya huduma takatifu ambayo Washiriki
hawana budi kuitekeleza kama Bwana Yesu alivyo itekeleza alipokuwa hapa Duniani
aidha aliongeza kuwa Watu wakimjua Mungu wataacha mabaya na Watamwekelea
Mungu,wataacha mabaya na Wataishi kwa Amani na Upendo kama alivyo agiza Bwana
Yesu.
Wakili wa mali ya Bwana
wa kanisa hilo Gregory Mbeba alisema kuwa lengo la kuaandaa harambee hiyo ni
kutokana na Waumini kuzidi uwezo wa kanisa wa kuchukuan waumini 400 kwa sasa
ambapo wamefikia waumini 2160 na swala ambalo linasababisha waumini wengine kusalia
Nje ya kanisa huku wengine wakuwa ndani ya kanisa.
“Tunaomba wadau
wote wapenda maendeleo kujitokeza kwa wingi kuja kuchangia kanisa
letu na watabarikiwa na Bwna Mungu na kufanya hivyo kutatusaidia kukamilisha
ndoto zetu za upanuzi na ukarabati wajengo la Kanisa ili kukidhi mahitaji ya
Kanisa” alisema Mbeba.
Kanisa hilo limekisia
kukusanya Tsh 100,000,000 katika harambee ambayo inatarajiwa kufanyika hapo
September,09 mwaka huu na kuwa katika jitihada za kanisa hilo zimekwamakutokana
na uwezo mdogo ambapo wameomba wadau kujitokeza na kutoa michango yao kkwa
lengo la kufanikisha na kuondoa usumbufu uliopo.
………….....mwisho…………