WANANCHI WA KIJIJIJCHA MIRARE WILAYANI RORYA WAMWOMBA MBUNGE KUMALIZA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI:



Rorya:
WANANCHI WA KIJIJIJCHA MIRARE WILAYANI RORYA WAMWOMBA MBUNGE KUMALIZA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI:

Wananchi wa kijiji cha Marongo kata ya Mirare Tarafa ya  Girango Wilayani  Rorya Mkoani Mara wamemwomba Mbunge wa Jimbo la Rorya Bw:Lameck Airo kuwasaidia katika kutatua Changamoto zinazo wakabili katika kijijin hicho kwa lengo la kuendeleza kukuza Uchumi.

Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Mtendaji wa kijiji katika kusoma risala ya Serikali ya kijiji Bw:Lameck Gebwa kwa niaba ya Wananchi wa kijiji cha Marongo mbele ya Mbunge katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya shule ya Msingi Ingri Chini kwa lengola kukusanya Maoni ya Wananchi kutoka katika Vijiji sita vinavyozunguka Ardhi ambayo imekuwa na Mgogoro takribani Miaka Kumi na Tatu kati ya Kampuni ya UDAFCO na Ushirika wa UMONI huo ni  Umoja wa Vijiji sita Vinavyozunguka Ardhi hiyo.

Wananchi hao walisema kuwa Changamoto hizo zimazowakabili hivyo wameomba  mbunge kama Mwakilishi wao kuweza kumaliza changamoto ikiwa ni pamoja na kutetea haki zao za msingi na kuweza kupat Mwafaka wa  kurudishiwa Ardhi yao mikononi wa Wananchi hao kwani wamnyanganywa na Mwekezaji kutoka katika kampuni ya UDAFCO.

Wananchi hao kupitia Serikali ya kijiji wametaja changamoto
 kuwa kijiji hicho kinakabiliwa na Ukosefu wa maji safi na salama, kumalizia Nyumba ya  katika shule ya Msingi Nyamwale kwani Wananchi hao wametumia nguvu zao na kuisha njiani, na kutengeneza Bara bara ya kutoka katika Kanisa la kisabato lililopo katika kijiji cha Marongo mpaka Mto Moli.

Sanjari na hayo ili kuweza kupata suruhisho la Mgogoro huo kati ya Wananchi wa Vijiji saba Mbunge huyo  ameamua kuzunguka katika vijiji sita kwa kushirikiana na Kamati yake, kamati ya halmashauri ya Wilaya hiyo pamoja na Wanasheria wa Serikali na kujitegemea uku Wananchi wananchi wakipiga kura ya wazi kuhusu shamba hilo kuzidi kumilikishwa na wawekezaji bilia Wananchi kupata feaida yeyote.

Katika kijiji cha Mirare wananchi  176 wamepiga kura wakitaka kurudishwa kwa shamba hilo  na wananchi 15 hawakupiga kura na 2wamependekeza A ksilimia kubwa kwenda kwa mwekezaji ili kumalizikia kwa Migogoro hiyo na mpaka sasa tayari amezunguka takribani Vijiji vinne akifanya Mkutano wa hadhara  ili asilimia kubwa ya kura wanadai kurudishwa kwa shamba hilo na kuweza kuendeleza kilimo chao kwani kilimo ndo Mkombozi wao.

Mbunge huyo Lameck Airo alisema kuwa yeye yuko tayari kuungana na asilimia kubwa inayoitaji haki  na kuweza na kuweza kufikisha Maoni ya wananchi hao kutoka Vijiji sita kwa Waziri  huska na kuweza kupatikana kwa Mwafaka kuhusu shamba hilo kurudi kwa wananchi au Mwekezaji

Babada ya kumalizika kwa Mkutano wa Kijiji cha Mirare kata ya Mirare Tarafa Girango Msafara wa Mbunge uliweza kuelekea katika   Mkutano Mwingine kwa ajili ya kuendelea kukusanya Maoni ya wanachi ili waweze kurudishiwa Ardhi yao inayomilikiwa na Mwekezaji na Mkurugenzi wa Kampuni ya UDAFCO Bw: Otieno Igogo.

Kwa upande  wa  wananchi wa kijiji cha Nyanduga wamepiga kura za wazi ka vijiji vingine Wananchi 6 wamependekeza Mwekezaji kupata asilimia kubwa kuliko Mwananchi na Wananchi176.

Aidha Mbunge huyo amekemea a suala zima la Wizi wa mifugo pamoja na kushirikiana na na kukanya baadhi ya Wananchi wanaoshirikiana na wezi wanaopitisha mifugo baada ya kuibwa katika vijiji jirani na kuongeza kuwa Maoni hayo ua Wananchi zitatengenezwa nakala nyingi na kuweza kurudishwa kwa Wananchi zikiwa na Miuri ya Mbunge kwa lengo la kupitia yale waliyoyasema katika Mikutano hiyo.


Powered by Blogger.