Halmashauri ya Mji wa Tarime yapitisha sheria ndogo.



Halmashauri ya Mji wa Tarime yapitisha sheria ndogo.



KIKAO cha  Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara juzi
wamepitisha sheria ndogo ndogo zitakazoiongoza halmashauri hiyo kwa
ajili ya kusimamia utekelezaji wa shuguli za maendeleo.
Sheria hizo zimetungwa mda mfupi baada ya halmashauri hiyo kupanda hadhi
kutoka Mamlaka mji
mdogo wa Tarime na kuwa halmashauri ya Mji  ambapo awali ilikuwa Mamlaka ya Mji mdogo wa Tarime ambapo walikuwa wakitumia sheria za halmashauri
ya Wilaya Tarime wakati ikiwa inaongozwa na viongozi wake Chirstoph
Mwita Mantago kama mwenyekiti na Hashimu Balongo akiwa katibu.

Akiongea kwenye
Baraza la Madiwani Mwanasheria wa halmashauri ya Mji wa Tarime Tumaini
Kigombe alisema kuwa halmashauri yake haina budi kutunga sheria ndogo
ndogo ambazo zitakuwa zinaiongoza na kuondokana na zile ambazo
zilikuwepo za halmashauri ya Wilaya.

Mwanasheria Kigombe alisema
mbele ya Baraza hilo kuwa taratibu zote za kisheria zimezingatiwa na
makundi na taasisi mbalimbali wametoa maoni kwa kuzingatia taratibu za
utungwaji wa sheria.

''Katika kutunga sheria ndogo tumezingatia
mazingira ya Soko kwa maana kuwa usafi unaofanyika na mabo mengine
ilikupata fedha za kuendeshea kuwalipa vibarua walinzi wa soko sanjari
na kulipa maji na Umme ndani ya soko na wala sio kuvunja sheria kama
inavyo daiwa''alisema Kigombe.

Aidha Kigombe alifafanua kuwa
maeneo yatakayoguswa na sheria hizo ni maeneo yote ambayo yatakuwa ndani
ya mipaka ya halmashauri ya Mji wa Tarime kama itakavyo
ainishwa.

Kigombe aliongeza kuwa shewria hizi ndogo zitakuwa
sheria za halmashauri wa Mji wa Tarime punde zitakapo tangazwa katika
Gazeti la Serikali pia zitatumika Eneo lote lililo chini ya mamlaka ya
Mji.

Aidha Kigombe aliongeza kuwa ada ya uzoaji taka chini ya
kifungu cha 28 Nyumba za kuishi au makazi kwa kaya kiwango cha ada kwa
mwezi kitakuwa Tsh 1,000 Nyumba za kulala wageni Tsh 2,000 mgahawa Mama
Baba lishe Tsh 1,000 pamoja na maduka Tsh 1,500.

''Eneo lingine
ni Hotel,Baa,Grosary Tsh 2,000,Vibanda au meza za biashara 1,000,Wachoma
chips,kuku,nyama saluni za kusuka na kunyoa nyweleTsh 1,500 mafundi
cherehani,samani za Gareji Tsh 5,000,wauza mbao au karakana za kuranda
mabo Tsh 5,000Ofisi au taasisi 3,000''alisema Kigombe.

Mwanasheria
huyo alimaliza kwa kusema kuwa Mtu yeyote atakaye vunja sheria hizi
ndogo atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atachukuliwa hatua
za kisheria ambapo atatakiwa kulipa faini isiyo
zidi Tsh 50,000 au kifungo kisicho zidi miezi 12 jela kutumikia ama
adhabu zote mbuli kwa pamoja.

Katika kikao hicho madiwani wa
kambi ya Upinzani walipingawakiongozwa na   mwenyekiti wao Charles ndesi
Mbusoro wa kata ya Turwa walipinga kupitishwa kwa sheria hizo na kuwa
zinawagandamiza Wananchi.

Aidha Madiwani wakambi ya Upinzani
walidai kuwa kuna baadhi ya sheria zilisha futwa na hazipaswi kurudiwa
katika makusanyo ya mapato kwani kufanya hivyo ni kosa na ni
kuwanyanyasa wananchi wa kipato cha chini.

Ndesi alisema kuwa
sheria hizo hazikupita kujadiliwa na Wanachi katika maeneo mbalimbali
kama ilivyo badala yake zimekuja kupitishwa katika Baraza ili kubarikiwa
na kupelekwa katika ngazi huisika na kutangazwa katika Gazeti la
Serikali tayari kutumika na kufanya hivyo Wananchi wataumia aliongeza
kusema.


Powered by Blogger.