Mhubiri wa kimataifa azawadiwa upanga:
Mchungaji Thobias Oluoch akikabidhi awadi ya chungu kwa mama mchungaji baada ya kukabidhi zawadi ya upanga mhubiri wa kimataifa Dr Egon Falk katika mkutano wa injiri unaofanyika viwanja vya serengeti mjini Tarime
Mhubiri wa kimataifa
azawadiwa upanga:
Mhubiri wa kimataifa kutoka Denimarka Dr Egon Falk
amezawadiwa upanga katika mkutano wa
Injiri unaotarajia kuanza Juni 25 hadi Juni 29 Mwaka huu katika viwanja vya
Serengeti Mijini Tarime uku miujiza mbalimbali
ikitendeka pamoja na upnyaji.
Katika kukabidhi zawadi hiyo iliyoandaliwa na Kamati ya
Maandalizi Mwenyekiti wa mkutano huo
Mchungaji Thobias Oluochi wa kanisa la Nazareti alisema kuwa upanga uo ni ishara ya kumkaribisha mgeni huyo kwa
lengo la kutumia upanga ili kuweza
kukata roho chafu.
“Tumekupa upanga huu utumike kutaka roho chafu ambazo
zitaweza kusogelea mkutano wetu pia tunatoa chungu kwa Mama mchungaji kama ishara yakuendeleza tamaduni za kiafrika chungu kitatumika kupika chakula cha
bwana” alsema Mchungaji oluochi katika kukabidhi zawadi hizo.
Mchungaji huyo aliongeza kuwa zawadi hiyo itakuwa yakwanza
kwa Mhubiri huyo wa kimataifa nakumtaka kuitumia vyema katika kukata roho chafu
kwa lengo la kuleta yaliyomema ndani ya
wilaya ya Tarime.
Dr Egon alisema kuwa wanatarimea wategemee miujiza kutoka
kwake kakribani siku tano ndani ya viwanja
vya sababa nakusema kuwa amependezzwa na kuwepo kwa viongozi wa kike katika wilaya ya Tarime.
“Nakumbuka miaka
arobaini iliyopita hapakuwa uongozi wa mwanamke nashukuru mwenyezi mungu abagui
kila mtu awe mwafirika muzungu,kila mtu anaweza kuongoza katika jina la yesu”
alisema Dr Egon.
Hata hivo Mhubiri huyo aliwataka wakazi wote wa Tarime wenye
dini wasikuwa na dini kuuzulia mkutano huo wa hadhara kwa lengola kusikia
nenola bwana ili wagonjwa,Vipofu, Virema waweze kuponywa kwa nguvu za mwenyezi
mungu.