Vijana watakiwa kumrudia Mwenyezi mungu:
Vijana watakiwa
kumrudia Mwenyezi mungu:
Rorya.
Vijana Wilayani Rorya mkoani Mara wametakiwa kumrudia
mwenyezi mungu ikiwani pamoja na
kuondokana na suala la wizi wa mifugo ambao umekuwa kero wilayani humo.
Kauli hiyo imetolewa na mbunge wa jimbo la Rorya Bw:Lameck Airo katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha utegi wilayani humo, kwa lengo
la kuzungumzia mgogoro wa ardhi kati ya Umoja wa vijiji sita vinavyozunguka
ardhi hiyo (UMONI) mwekezaji wa kampuni ya(UDAFCO)chini ya usimamizi wa
mkurugenzi wake Otieno Igogo.
Lameck alisema kuwa vijana waliowengi wamekuwawakijiusisha
katika suala la wizi wamifugo na uku wengine wakiusika kukaribisha waharifu
kutoka wilaya jirani na kuiba mifugo hiyo.
“Kijiji cha Utegi kuna kijana mmoja na Nyanduga kuna vijana
wawili natoa agizo kwa serikali za vijiji kuitisha mikutana ili niweze kuleta
kijana mmoja ambaye amejisalimisha na kuanza kuwataja wezi ili wakamatwe”
alisema Lameck.
Aliongeza kuwaendapo vijana hao watamtumikia mwenyezi mungu
itasaidia kuwabadili tabia na kuondokana na suala la wizi wa mifugo kwani
limewanyima amani wakazi wa Rorya na Vijiji vyake.
Aidha mbungea huyo alisema kuwa asilimia kubwa ya wakazi wa
rorya ni wafugaji hivyo mifugo hiyo utumika kuwasomesha watoto endapo wizi
utaendelea watoto hawanda shule kwani kipato kinapungua kutokana na wizi huo.
Sanjari na hayo kutokana na Mgogoro wa ardhi ambao umekuwepo
takribani miaka kumi na tatu kati ya wananchi na mwekezaji ameamua kuzunguka
katika vijiji sita kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi uku wakipiga kura
za wazi ili waweze kuwasilisha maoni hayo kwa waziri mwenye dhamana kwa lengo
la kutatua mgogoro huo.
“Tumemaliza mzunguko wa vijiji vyote tumepata maoni ya wananchi wanaoteseka
tunaenda kuyafanyia kazi asilimia kubwa
kulingana na takwimu tuliyopata kutoka kwa wananchi na wamedai kurudishiwa ardhi yao ili waweze
kulima au kuleta mwekezaji mwinginea ambaye atawanufaisha” alisema Mbunge.