Majipu, kizunguzungu kwa waliokunywa dawa ya Sangoma Tarime
Majipu,
kizunguzungu kwa waliokunywa dawa ya Sangoma Tarime
Tarime.
Hali ya
walionaswa baada ya kunywa dawa ya “Sangoma” mei saba mwaka huu katika kijiji
cha Kenyamanyori Wilayani Tarime si ya kutilia matumaini ijapo kwa kwa sasa
wanajitambua na kuongea, wamekumbwa na dhahama ya mlipuko wa majipu na kuishishiwa
nguvu mwilini.
Waathirika
hao wameeleza kuwa hawana nguvu ya kufanya kazi, kama ilivyo kuwa mwanzoni hali
inayowafanya hata familia zao kuathirika kiuchumi na zinakula kwa shida.
Wawili
kati ya wanane walionaswa na dawa ya mganga kutoka Busia Kenya mei 7 wameeleza
na kuwa majipu yameenza kuwatokea sehemu mbalimbali za miili yao na kuwafanya
waingiwe na hofu ya uhawao.
Mwananchi
lilipata kukutana na Moya Mwita 29 aliyesema kuwa alipata fahamu baada ya siklu
tatu akiwa kwa mganga katika eneo la Karugekere Bunda na alikaa huko wiki nzima
akipata matibabu.
“Daada
ya siku tatu ndio nilipata fahamu nikiwa kwa mganga huko Bunda, lakini
nilimaliza wiki nzima bila kupata choo kubwa, wakati huo sikuwa na hamu ya kula
chakula chochote isipokuwa maziwa na uji waliokuwa wananilazimisha kunywa”
alisema Mwita.
"Nakuongeza:
“Kutokana
na (sumu) dawa ile nimeanza kutokwa na majipu hata hapa nilipo ninaumwa”
alionyesha Mwita wakati akieleza majipu yalitomtokea.
Makoromu
Nyangera 48 yeye alikiri kuwa na hali mbaya kiafya na kuwa kila siku inapofika
usiku tumbo humvuruga, hapendi kusikia kelele na mwanga mkali ambavyo alisema
vinamsabaisha kichwa kuwa katika hali mbaya.
“Ukifika
usiku saa 11 alfajiri tumbo linaunguruma hali ambayo zamani haikuwa hivyo,
njiani nikitembea naona bahari, kizunguzungu. Hali hiyo ikitokea natamani nikae
sehemu tulivu nipumzike au nilale” alisema Makoromu, akaongeza:
Nguvu
yangu ya zamani imeisha, nilikuwa nafanya kazi ya shamba saa nane lakini kwa
sasa ni saa mbili tu nimechoka, nimepata pigo … familia yangu inakula kwa
kusuasua maana nimetumia mtaji wote kujitibu ingawa mpaka sasa walikuwa
wananihudumia hawaniambia wametumia kiasi gani…. Mimi nilipelekwa Mwanza”
alisema.
Ayubu
Wambura aliyeibiwa alisema kuwa watu hao
hawaonyeshi dalili za kumrudishia mali yake na kuwadhahadhalisha kuwa isije
ikafika sehemu wakamlaumu .
“Waliniibia
na kumuua mke wangu wameonekana wazi lakini hawataki kunirejeshea gharama na
mtaji wangu, wasije wakanilaumu kwa mengine yanayoweza kutokea hapo baadaye”
alisema Wambura’
Hata
hivyo wananchi walieleza kuwa walionaswa na dawa ndio wahusika wa tukio la
kuibiwa kwa Wambura kinachotakiwa wamlipe kiasi alichotaka ili kupunguza matatizo
yanayoweza kutokea baadayes.
"Walionaswa
na dawa ndio wezi , anayewapa kichwa ni usalama wa taifa aliyeko Dar salaam
ambaye mdogo wake alinaswa na ndiye aliyeagiza Wambura akawekwa ndani siku tatu
akitishia kuwa mdogo wake akifa “ alisema mmoja wa wanakijijis(Griady rioba).
Hakutaka jina lake liwe gazetini.
Awali
kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Tarime Rorya Justus Kamgisha alisema kuwa
kinachofanywa ni mganga kuwekwa hatiani kutokana na kitendo alichokifanya kwa
kuwanywesha wananchi dawa.
“ Watu
hawa wanamakasa na kama jeshi la polisi mtuhumiwa hayupo alisha kimbilia kwao
Kenya ili kulishughulikia hili lazima apatikana ” alisema Kamgisha.