Mama akana mtoto wake kituo cha polisi
Mama akana mtoto wake kituo cha
polisi
Tarime:
Mkazi wa
Sirari anashikiriwa na jeshi la polisi katika kituo cha polisi Sirari kwa
kumtelekeza mtoto wake wa kuzaa mwenye umri wa miezi sita aliyetajwa kwa jina
la Gloria Lucas.
Binti huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mariam
mwita mwenye umri wa 16 alimtelekeza mwanaye
juni 7 katika kijiji cha Gwitiryo kata ya Nyamaraga Wilayani Tarime kwa kumpeleka kwa mzazi mwenza kisha kumwacha
nje ya geti majira ya usiku.
Akitoa
maelezo kituoni hapo juni 9, Mariam alisema kuwa hataki mtoto na ndiyo maana
aliamua kumpeleka kwa baba yake ili awe katika mikono salama badala ya
kumpeleka sehemu nyingine.
Mariamu
anayeishi Sirari katika nyumba ya wageni iitwayo MK aliondoka nyumbani kwao
mwaka 2010 akiacha masomo ya shule ya msingi, baada ya kuwashinda wazazi wake waliokuwa wakimkanya
kuacha tabia yake mbaya.
Alikimbilia mji
mdogo wa Sirari na kuamua kuwahudumia wanaume kimwili kila walipojitokeza
kutaka huduma yake hadi hivi sasa alipoona mwanaye Glory anambana kutoa huduma
hiyo na kuamua kufanya unyama huo wa kumtelekeza akingali akihitaji maziwa na
yake.
“Sitaki
mtoto ananibana na shindwa kuwahuru kufanya mambo yangu” alisema mtoto huyo
wakati wa mahojiano.
Hata
hivyo alikutana na Lucas Muhiri 17 ambaye ni baba yake na mtoto Glory mwaka
2012 na kuamua kuanzisha mahusiano Wakiwa katika kijiji cha Kebeyo ambapo walipeana ahadi ya kuoana
na kuanzisha mahusiano wakati wakijiandaa kutimiza ndoto yao ya kuwa mume na
mke ijapo umri wao ulikuwa bado wa utotoni.
Muhiri
akiwa na mtoto wake alisema kuwa wakati wakijiandaa kuitimiza ndoto yao mwaka
jana januari, dada yake aliuagua na kumwita kwenda mwanza kumwangalizia mji ili
aende kwenye matibabu Dar Salaam na
aliporudi hawakuwa na mawasiliano tena tangu mwezi wa pili kwaka huu.
Hata
hivyo Muhiri ambaye kwa wakati huo alikuwa kinyozi katika kitongoji cha
Nyantaburo katika kijiji Kebeyo amekiri kuwa mtoto ni wake na kumpokea kumlea
kwa kukabidhiwa na serikali ya kata na polisi kimaandishi baada ya kuonekana
kuwa hakuna sehemu nyi ngine salama atakapopelekwa isipokuwa kwake.
Mama
aliyemwokota mtoto Gloria, Rhobi Muhiri (55) amesema aligundua kuwa kuna mtoto
nje ya geti baada ya kuambia na mjukuu wake mwenye miaka 6 aliyemtaja kwa jina
Wambura Nyamohanga majira ya kati ya saa moja ama saa mbili usiku lakini
hakuamini hadi alipomsikia akilia.
Rhobi
alisema kuwa baada kufika getini hapo alimkuta mtoto amefunikwa kitambaa bila
nguo nyingine pembeni kukiwa na nguo zake na unga wa ule, huku akionekana kuwa hajala kwa muda fulani, ambapo
alimchukuwa na kumpeleka ndani kumwandalia uji.
Alilala
naye hadi kesho yake juni 8 alipoenda kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji
lakini hakumkuta na kuacha taarifa kwa mke wake. Aliondoka kwenda kituo cha polisi sirari na kutoa maelezo juu ya mtoto huyo na
kuambiwa arudi naye kesho yake kwa makupewa maelekezo zaidi.
Baada ya taarifa kusambaa mji mdogo wa Sirari mama
yake na mtoto alifahamika na baba yake pia kufahamika , “Kumbe alikuwa mjuu
wangu” alisema Muhiri.
Awali
mwenyekiti wa kijiji cha Sirari Nyangoko Romani alisema kuwa siku ya jumapili
akitoka kanisa aliitwa na mtoto akimwambia kuwa kuna mtu anamuita kwenye nyumba
ya kulala wageni ya MK alipoenda aliwakuta watu wamejaa wamemzunguka binti
huyo.
Baada ya
kuhoji aliambiwa walikuwa wanamshuku Mariamu kutokuwa na mtoto na walihitaji
awambie alikompeleka lakini akikana kutosema chochote.
“…alikataa
kusema alipo mtoto nilipokuwa nikimuuliza, nikamzaba kofi akaomba kusema name
nikamwamrisha aseme alipo mtoto wake ndipo aliposema alimpeleka Kijiji cha
Gwitiryo na kumwacha huko. Wakati huo taarifa zilikuwa zimesikika za mtoto
kuotokotwa kijijni hapo” alisema Romani.
Afisa
maendeleo wa kata ya sirari Gabriel Nguvava amesema kuwa kutokana hali ya kata na Wilaya kukosa kituo
cha kulelea watoto wadogo wameamua kumkabidhi mama Mhuiri mtoto ili kuendelea
kuwa katika miko salama.
“Matukio
ya ukatili katika Mji wa sirari
ni kati ya asilimia 80-90 ikionenyesha kuwa kuna haja ya serikali kutoa elimu juu
ya umri rika ili wanapoingia katika mahusiano na kukutwa na mimba,wajue njia sahihi ya kutatua matatizo yao ni kufika
katika dawati la jinsia ofisi za maendeo ya jamii na kwa ushirikiano wa dawati
la jinsia la polisi matatizo yatatauliwa na si kuwatelekeza wanao”.
Mratibu dawati
la jinsia kituo cha Polisi Sirari Veronica Alphonce alisema kuwa suala hilo
lilikuwa ngazi ya kituo hakupenda kulizungumzia kwa kuwa yeye si msemaji ijapo walikuwa
wanatafuta jinsi ya kufanya kushughulikia
tatizo la binti huyo kwani kitendo alichokifanya kilikuwa ni kibaya, kwa umri
wake hakutakiwa kuwa na mtoto.
“Matukio
haya ni mengi eneo hili la Sirari kutokana na mwingiliano wa wageni wengi,
tunapata vyesi vingi kila siku” alisema Alphonce .
ATT:
Rhobi Muhiri (55) akiwa amebeba mtoto Glory aliyemwokota getini kwake baada ya
kutelekezwa na Mariam Mwita 16 .
2.Lucas
Muhiri (17) na mama yake Rhobi Muhiri akiwa amembeba mjukuu wake baada ya
kukabidhiwa kimaandishi na ofisi ya maendeleo ya jamii kata ya Sirari na mbele
ya jeshi la Polisi kumtunza mtoto huyo.
Mwisho.