Mwenyekiti, VEO wanusurika kipigo wajumbe serikali ya kijiji:
Mwenyekiti, VEO wanusurika kipigo
wajumbe serikali ya kijiji
Kikao
cha serikali ya kijiji cha Sirari kilishindwa kuendelea baada ya wajumbe kudai kukerwa
na kauli ya mwenyekiti wa kijiji hicho Nyangoko Romani kwa kuwambia wajum be hao kuwa
ajenda ya kupitisha bajeti haitakuwepo maana wevyeviti wa vitongoji
hawakupeleka bajeti yao.
Hali hiyo
ilizua taharuki ndani ya kikao na kuwafanya wajumbe kuanza kurushiana matusi na
kutishiana kiasi cha kupigana makonde hali iliyokifanya kikao kukatishwa muda
mfupi baada ya kuanza. Sauti zilisikika zikisema “tunataka posho yetu huwezi kutuita hapa kupanga
bajeti na posho yetu tusipate”
Wakiongea
kwa jabiza juu ya kuomba fedha yao ya malipo ya mwaka mzima kwa wenyeviti vitongoji ambayo ni sh, 60,000, mmoja wao aliyejitambulisha kwa
jila la Robert Mashon alisema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakiambiwa kupewa
posho, na sasa kijiji kimepata fedha kutoka Halmashauri ya Wilaya ya sh, 2.5 milioni.
“Fedha
imekaa banki inaendelea kupungua ikikatwa bila kutumika, tupewe posho yetu ya mwaka sh, 60,000 na nyingine tuingize
kwenye matumizi ya kijiji kuliko kukaa humo inaendelea kukatwa” alisema Robert.
Na
kuongeza kuwa, mkutano wa serikali ya kijiji uliitwa ili kupanga bajeti, lakini
baada ya kusaini mahudhurio mwenyekiti aliswambia kuwa ajenda ya bajeti isubiri
kwanza hadi hapo wenyeviti hao watakapoonyesha katika vitongoji vyao wanataka
kufanya nini ili wapewe fedha hizo.
Hata
hivyo Nyangoko Romani alisema kuwa wenyeviti wa vitongoji hawakuwa na bajeti ya
vitongoji vyao hivyo ikaonekana kuwa watakapo pewa fedha hizo watazitumia
kinyume na kuwaomba waandae bajeti yao
itakayoonyesha kiasi cha fedha wanachokitaka na kinaenda kufanya nini ndipo
wapitishe bajeti ya kijiji hicho.
“Wanapoitwa
kwenye shughuli za maendeleo hawaji na pengine huja mmoja leo wamesikia mkutano
wa bajeti wote wamefika, tena kwa kupigiana simu, na cha kushangaza hawakuwa na
bajeti ya vijiji vyao” alisena Romani muda mfupi baada ya kikao hicho kushindwa
kuendelea.
Mtendaji
wa kijiji hicho Mirumbe Mirume alisema kuwa kushindwa kukamilika kwa mkutano wa
serikali ya kijiji kunamfanya yeye ashindwe kutekeleza majukumu yake ipasavyoa
kwani anaitegemea serikali hiyo kupitisha maamuzi ili yeye ayafanyie kazi.
“Nashindwa
kutekeleza majukumu yangu kutokana na wajumbe hawa kutokuwa makini kufanya
maamuzi, na wakati mwinmgine naweza nikaonekana mimi ni mzembe.
Hata
hivyo mtendaji wa kata hiyoa ya Sirari Paulo Maisori alisema kuwa Sirari ni
moja ya kata ambazo watu ni wabishi na wakali wanapotakiwa kufanya shughuli za
maendeleo.
“Nimepita
katika kata na vikao vya serikali za vijiji nyingi lakini sijawahi kuona kijiji
kama hiki, watu ni wabishi ukiongea wanaamka wanataka kukupiga badala ya
kuangalia maendeleo ya kijiji chao,
kushindwa kufanyika kwa kikao hicho kwa kumshabulia mwenyekiti na mtendaji ni
kwa sababu wamekuwa wakaidi wao wanadai
posho yao y ash, 5000 kila mwezi kwa mwaka mmoja sh, 60,000 bila
kuonesha juhudi za kushiriki katika maendeleo” alisema Maisori.
……..MWISHO….