JAMII YA KIKURYA YAIMIZWAKUSOMESHA WATOTO ILI KUPATA FURSA ZILIZOPO NDANI YA WILAYA
Picha ya
Mgeni rasmi Katibu Tarafa wa Inano Bw: Marwa Chaha kwa niaba ya Mkuu wa
Wilaya ya Tarime John Henjewele akitoa hotuba yake katika Maadhimisho ya
Mtoto wa Afrika yaliyofanyika kiwila katika kata ya Muriba Tarafa ya
Ingwe uku kauli mbiu ikisema kuwa kupata Elimu bora na Isiyo na Vikwazo ni haki ya kila Mtoto
Jamii ya kikurya imeimizwa
kusomesha watoto kwa lengo la kuweza kupata ajila kupit ia fursa zilizopo katika katika wilaya ya Tarime
ususani mgodi wa dhahabu uliopo Nyamongo wilayani humo.
Kauli hiyo imetolewa na Mgeni
rasmi katibu Tarafa wa Inano BW:Marwa Chacha
kwa niabaya ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime John Henjewele katika
maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya katika kata ya Muriba Tarafa ya Ingwe Wilayani humo,
uku kaulimbiu ikisema kuwa Kupata Elimu bora na Isiyo na Vikwazo ni haki ya
kila Mtoto.
Mgeni rasmi alisisitiza suala
zimala Wazazi Walezi kuwekeza katika
suala zima la Elimu ili Watoto wawezekuondokana na uvamizi wa mara kwa mara katika Mgodi wa North
Mara na kupelekea baadhi ya watoto koteza Maisha yao na wengine kuwaVilema wa
kudumu kwa kupigwa Risasi katika
Mapambano baina ya Jeshi la Polisi.
Alieleza kuwa suala zima la
kushuka kwa Elimu na kutoroka kwa wanafunzi na kuacha shule na kujiingiza
katika suala la uvamizi wa mgodi ni
mwamko mdogo wa wazazi na walezi katika Elimu.
“Wazazi tuungane kwapamoja
kupambana na Ukatili dhidi ya Mtoto kumpa haki yake ya kupata elimu na kila
mmoja wetu kutimiza wajibu wake ikiwa ni pamoja na kuondokana na kuozesha
watoto mambo hayo yamepitwa na wakati” alisema Mgeni rasmi.
Hata hivyo Mgeni rasmi
aliongeza kuwa kupitia Serikali wameunda mikakati mizuri ya kuanzishwa kwa
vikundi vya ulinzi shirikishi kupitia jamii inayozunguka mgodi huo ili kuweza kupunguza Mauaji yanayotokea katika Mgodi huo ikiwa ni moja ya kupatikana kwa ajila kwa vijana hao.
Katika maadhimisho hayo Ofisa
Maendeleo Bw Charles Ouma kwa niaba ya Ofisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya
Tarime Bi:Dorotty Jovin amezitaja Takwimu zinazomugusa mtoto katika suala zima la
Ukatili kuwa katika Mei mpaka juni Ndoa za utotoni zimeripotiwa 2 Mimba7
Ubakaji11 kurawiti1 shambulio kwa watoto7, utoroshaji wanafunzi 39 nakusema kuwa
jumla yameripotiwa matukio 69 katika ofisi ya Ustawi wa jamii nakuitaka jamii
kutoa taarifa pale matukio yanapojitokeza.
Katika kusoma Risala mbele ya
Mgeni rasmi watoto hao katika kupigania
haki yao wamezitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni kubaguliwa kwa watoto wa
kike katikafamilia ikiwa ni pamoja na kunyimwa haki ya kupata Elimu wazazi uwaozesha watoto hao ili kupata
kipato, kushawishiwa katika suala zima la
Ukeketaji suala ambalo ni hatari kwa afya,kuzidi kuongezeka kwa matukio
ya kikatili dhidi ya mtoto wa kiafrika kupitia wazazi na walezi wao.
“Wazazi unganisha nguvu ya
pamoja ili kutokomeza vitendo vya kikatili ikiwa ni pamoja kutoa kipaumbele na
wekeza katika suala zima la Elimu na si kufikiria na kuwaza Mali za
kutuozesha bali tuozeshe katika Elimu” walisema Watoto hao.
Hata hivyo kupitia Maadhimisho hayo watoto hao wameiomba
serikali kuangalia haki za mtoto na kumpa kipaumbele kwa lengo la kujikomboa,
kupinga ili kukmesha suala zima la ukeketaji, kukomesha ajila za watoto na
kuodheshwa katika umri mdogo.
Sanajari na hayo jamii
imeimizwa kuanzisha suala zima la Mapambano katika kupinga ukatili wa Mtoto
kuanzia katika ngazi ya kaya,ili kuweza kutokomeza suala zima la Ukatili dhidi ya Mtoto, ikiwa
ni pamoja na kuondokana na Uvamizi wa Mugodi wa African Barrick Golg ABG North
Mara.
Kwa upande wake ofisa
Ushirikishwaji kutoka katika Mgodi wa African Barrick Gold ABG Bw: Nikodemus
Keraryo alisema kuwa Mgodi huo kwa kutambua
umuhimu wa Mtoto wanazidi kutekeleza miradi ya jamii kama
vile ujenzi wa Shule,Zahanati.Barabara na huduma nyingine.
“Tunatambua Umuhimu wa watoto
hivyo tutazidi kusaidia jamii kupitia idara ya Mahusiano” alisema Keraryo.
Aidha Mgodi huo ili kuongeza
hamasa katika suala zima la Elimu wamesema kua katika Wiki mbili mbeleni
wataweza kupita katika shule 16 za Msingi zilizomo katika Vijiji vinavyozunguka Mgodi huo na kutoa zawadi
mbalimbali kwa watoto waliofauru vizuri Mwaka huu na kuomba na mgeni rasmi kuwa
endapo wataanza zoezi hilo wahusishe viongozi wa serikali wakiwermo Maofisa
Elimu kwa lengo la kukutana na Wazazi
ili kuzungumzia chanagamoto katika suala zima Elimu hiyo.
…………Mwisho….