African Barrick Gold (ABG) ITAZIDI KUSAIDIA JAMII:
Ofisa Ushirikishwaji Bw:Nicodemus Keraryo akitoa shukrani zake kwa niaba ya Mgdi wa African Barrick Gold (ABG) katika Maadhimisho ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika ngazi ya Wilaya katika Kata ya Muriba Tarafa Ingwe:
Ofisa Ushirikishwaji kutoka katika Mgodi wa African
Barrick Gold ABG Bw: Nicodemus Keraryo alisema kuwa Mgodi huo kwa kutambua umuhimu wa Mtoto wanazidi kutekeleza miradi
ya jamii kama vile ujenzi wa Shule,Zahanati.Barabara na huduma nyingine.
“Tunatambua Umuhimu wa watoto
hivyo tutazidi kusaidia jamii kupitia idara ya Mahusiano” alisema Keraryo.
Aidha Mgodi huo ili kuongeza
hamasa katika suala zima la Elimu wamesema kua katika Wiki mbili mbeleni
wataweza kupita katika shule 16 za Msingi zilizomo katika Vijiji vinavyozunguka Mgodi huo na kutoa zawadi
mbalimbali kwa watoto waliofauru vizuri Mwaka huu na kuomba na mgeni rasmi kuwa
endapo wataanza zoezi hilo wahusishe viongozi wa serikali wakiwermo Maofisa
Elimu kwa lengo la kukutana na Wazazi
ili kuzungumzia chanagamoto katika suala zima Elimu hiyo.