DC TARIME AKEMEA SUALA LA UVAMIZI WA MGODI:
Katibu tarafa wa Inano
Bw:Marwa Chacha kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime John Henjewele amekemea
suala la Vijana kuvamia Mgodi wa dhahabu wa African Barrick Gold ABG North Mara,
suala ambalo linasababisha kupoteza kwa Maisha ya vijana hao baada ya kupata Dhahabu hizo
baadhi upelekea kuuana wakati wakinuyanganyana dhahabu hizo uku wengine
wakipigwa risasi na Jeshi la Polisi wakati wa kupambana kipindi
wakifukuzwa kutoka ndani ya Mgodi huo
nakupelekea kupoteza maisha na wengine kuwa vilema wa kudumu.
Kauli hiyo ilitolewa hivi
karibuni mbele ya Wazazi na Walezi katika Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika
yaliyofanyika kiwilaya katika kata ya Muriba Tarafa ya Ingwe,uku kaulimbiu ikisema
kuwa Kupata
Elimu bora na Isiyo na Vikwazo ni haki ya kila Mtoto.
Aidha Mgeni rasmi alisisitiza
wazazi kuwapatia Watoto wao Elimu ili waweze kuajiliwa ndani ya Mgodini huo
baada ya kupata sifa za kuajiliwa nasikutumia nguvu katika uvamia Mgodi huo.
“Mgodi siyo Mali ya Mzungu ni Mali ya Serikali kwa sababu
wanalipia kodi endelea kuhamasisha vijana wenu waondokane na kuvamia Mgodi na
wekezeni kwenye Elimu ili kunusuru vijana hao na suala la uvamizi litapungua” alisema.
Hata hivyo Mgeni rasmi
aliongeza kuwa wamejipanga kugawa maeneo ya wazi kwa lengola kuwanufaisha
Wachimbaji wadogo ili kuweza kupunguza suala la Uvamizi wa Mara kwa Mara ambao
ni Changamoto kubwa.
Vilevile mgeni rasmi
aliwataka wazazi na walezi kutoa ripoti katika vyombo vya dola pale vitendo vya
ukatili vinavyotokea ili kukomesha ukatili dhidi ya Watoto.
“Ofisi ziko wazi madawati ya
jinsia yapo na jeshi la polisi linafanya kazi vizuri toeni tarifa ili waharifu
wachukuliwe hatua mara moja” alisma Mgeni rasmi.
Kwa upande wake ofisa Ushirikishwaji
kutoka katika Mgodi wa African Barrick Gold ABG Bw: Nikodemus Keraryo alisema
kuwa Mgodi huo kwa kutambua umuhimu wa
Mtoto wanazidi kutekeleza miradi ya jamii kama vile ujenzi wa
Shule,Zahanati.Barabara na huduma
nyingine ili mtoto wa Afrika aweze kupata haki yake ya Msingi hususani
Elimu.
“Tunatambua Umuhimu wa watoto
hivyo tutazidi kusaidia jamii kupitia idara ya Mahusiano” alisema Keraryo.
Aidha Mgodi huo ilikuongeza
hamasa katika suala zima la Elimu mbele ya Mgeni rasmiwalisema kuwa katika Wiki mbili mbeleni wataweza kupita kila
shule kati ya shule 16 za Msingi
zilizomo katika Vijiji vinavyozunguka
Mgodi huo na kutoa zawadi mbalimbali kwa watoto waliofauru vizuri Mwaka huu na
ndipo Mgeni rasmia aliwataka viongozi wa Mgodi huokuwa rasmi endapo wataanza zoezi hilo wahusishe
viongozi wa serikali wakiwemo Maofisa Elimu
kwa lengo la kukutana na Wazazi ili kuzungumzia changamoto zilizopo katika shule hizo.