Wazee wa Mila Tarime watakiwa kusimamia Kauli zao kuhusu Kupiga Vita Uke...



Wananchi
wa kata ya Manga na Komaswa Wilayani Tarime Mkoani Mara Koo ya Bukenye
wakiwa katika Mkutano wa hadhara kwa lengo la kupewa Elimu ya Kupinga
Ukeketaji, Ndoa za Utotoni na Mimba za Utotoni kutoka kwa Wazee wa Mila
Muungano wa koo 12 kabila la Wakurya ambao wanaendelea na Mzunguko huo
ili kufikia Koo zote 12.


Wazee hao pia wanapiga Marufuku Mila
Potofu Miiko  ambayo inazidi   kukandamiza Mtoto wa Kike ambaye
hajakeketwa kuendelea kubaguliwa katika Jamii inayomzunguka.
Wazee
wa Mila koo ya Bukenye wakiwa katika Kikao cha pamoja kabla ya kwenda
kwenye Mkutano wa hadhara ili kutoa Elimu ya Kupiga Vita Ukatili dhidi
ya Mama na Mtoto.
Afisa
Tarafa ya Inano Marwa Rutta akiongea na Wazee wa Mila ambapo amewataka
Wazee hao kusimamia Kiukweli Kauli zao wanazotoa kuhusu suala la Kupiga
Vita Ukeketaji kwa Mtoto Wakike wilayani Tarime Mkoani Mara.

Nchagwa Mtongori Mwenyekiti wa Wazee wa Mila Muungano wa Koo12 akifafanua jambo katika Kikao hicho.

Diwani wa kata ya Manga Steven Gibahi akichangia jambo katika Kikao hicho cha Wazee wa Mila.

Mkutano wa hadhara kwa ajili ya kupiga Vita Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike kikiendelea katika Kijiji cha Bisarwi kata ya Manga




                              Wazee wa Mila wakitoa Elimu.


Sister
Stella Mgaya ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masanga ambao
wanapinga ukatili wa kijinsia akitoa Elimu na Madhara ya ukeketaji kwa
Mtoto wa Kike.


Abel
Gichaine ambaye ni Mratibu wa huduma za Afya na Ustawi wa Jamii Wilaya
ya Tarime akitoa Elimu juu ya  Madhara ya Ukeketaji kipindi Mama
anapojifungua na kusisitiza suala la Tohara Salama.


...Tazama video hapa Chini Kupata haabri Kamili...
Powered by Blogger.