Wazazi na Walezi Tarime wapewa Elimu juu ya Malezi ya Watoto wao



Wazazi
na Walezi Wilayani Tarime Mkoani Mara wakiwa katika Mafunzo
yaliyoandaliwa na Shirika la ATFGM Masanga Chini ya Ufadhili wa TERRE
DES HOMMES NETHERLAND (TDH) kwa lengo la kuendeleza malezi bora kwa
watoto wao pamoja na jamii inayowazunguka.

Mafunzo hayo
yameshirikisha Wazazi na Walezi 80 kutoka katika Kata 10 ili wawe
mabalozi wazuri wa kutoa Elimu ya malezi bora kwa watoto katika maeneo
wanayotoka ikiwa ni pamoja na kulinda Mtoto dhidi ya Ukatili wa kijinsia
Vikiwemo Vipigo, kuchomwa Moto, Kunyimwa Chakula pamoja na Kushindwa
kuwapatia Elimu bila kujali jinsia.

Valerian Mgani ambaye ni Meneja Miradi Shirika la ATFGM Masanga akifafanua jambo katika Mafunzo hayo.

Ostack
Mligo ambaye ni mwezeshaji wa Mafunzo hayo akielezea jambo katika
Semina hiyo baada ya wazazi hao kuunda Makundi ili kijibu Maswali.

                            Mafunzo yanaendelea.


Mmoja wa washiriki akichangia hoja katika Semina hiyo.


          Maswali yakijibiwa kupitia Vikundi mbalimbali.





Ashura Ayoub ambaye ni Afisa Ustawi wa jamii akieleza jinsi kitengo hicho kinavyosaidia jamii ambayo inakumbwa na Ukatili.

    Mmoja wa washiriki akiwasilisha kazi ya kikundi

....Tazama Video hapa Chini kupata habari Kamili.....
Powered by Blogger.