Rais Magufuli:Kilimo Kifanyiwe Mageuzi Ya Uchumi
Na Judith Mhina-MAELEZO
Mahitaji ya Soko la chakula Barani Afrika kwa sasa ni Bilioni 300 na Ifikapo mwaka 2030 itakuwa Trilioni moja.
Hayo
yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Joseph Magufuli wakati akizindua Mpango wa Programu ya Sekta ya Kilimo
ASDP 11 jana jijini Dar-Es-Salaam katika ukumbi wa Kimataifa Mwalimu
Julius Nyerere Conventional Centre.
Rais
Magufuli alisema nchi yetu ni kati ya nchi zenye bahati ya kuwa na
ardhi ya kutosha ya uzalishaji kwa njia ya umwagiliaji kwa kuwa tuna
vyanzo vingi vya maji. Hivyo ni lazima wakulima wetu kunufaike na fursa
hii ya kipekee iliyopo Barani Afrika.
Akizitaja
changamoto ambazo zikipatiwa ufumbuzi kutakuwa na mageuzi makubwa
katika sekta ya kilimo Rais Magufuli amesema “Kilimo lazima kiwe na tija
ambapo eneo dogo la kilimo linakuwa na uzalishaji mkubwa”.
Akitoa
njia za kufanya mageuzi hayo ya kilimo Rais ameongeza wakati umefika
vituo vyetu vya Utafiti vya Kilimo, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine – SUA
kuhakikisha wanafanya tafiti zinazolenga kuongeza jita katika mazao
yetu,
Aidha,
Maafisa Ugani waache tabia ya kukaa ofisini, waende kwa wakulima na
kuwashauri njia bora na sahihi zilizotokana na tafiti hizo ili Kuongeza
uzalishaji maradufu na kuchochea uchumi wetu kukua kwa kasi.
Amewaasa
watendaji wa sekta ya kilimo kuwa na matumizi mazuri ya fedha za
programu ambapo fedha zinazohitajika ni takribani shilingi za Tanzania
Trilioni 13.82 kati ya hizo Serikali na Washirika wa Maendeleo watatoa
asilimia 40 na Sekta Binafsi asilimia 60.
Rais
Magufuli ameagiza na kusema haiwezekani nchi za wahisani na wafadhili
mbalimbali watoe fedha zao, alafu utekelezaji wa program uwe hauridhishi
kwa kutenga fedha nyingi katika shughuli za utawala badala ya
kuelekezwa kwa walengwa.
“Programu
ni lazima itafute muarobaini wa masoko ya mazao ya kilimo mifugo na
uvuvi , hii ni pamoja na uwanzishwaji wa viwanda mbalimbali ambapo
itachochea zaidi wakulima kuzalisha kwa wingi na kuondoa adha ya
kutafuta masoko na kuwatia wakulima hasara” alisema Rais.
Akisisitiza
jambo hili Rais Magufuli amewaagiza Mabalozi wote walioko nje ya nchi
kuhakikisha wanatafuta masoko ya mazao mbalimbali katika nchi walizopo.
Hii ni mojawapo ya majukumu yao katika sehamu zao za kazi
Serikali
imefanya na inaendelea kufanya mazingira wezeshi ya kuhakkikisha mazao
yanatoka vijijini kwa urahisi kwa kujenga miundombinu ya barabara na
uwekaji wa umeme ili kuweza kuchakata mazao hukohuko katika sehemu za
uzalishaji na kuziongezea dhamani.
Serikali
kwa kushirikiana na sekta binafsi kuhakikisha inawekeza zaidi katika
kilimo na viwanda vitokanavyo na mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi. Sekta
binafsi ijipange na kuonyesha kwa namna gani itashiriki katika kilimo,
viwanda na kufanya tafiti zenyemanufaa katika kilimo.
Aidha
Rais Magufuli amenyooshea mkono na kuonyesha masikitiko yake kwa Benki
ya Kilimo Tanzania TAB kwa kushiriki kutowapa mikopo na kuwatenga
wakulima ambao ndio walengwa, na kutoa mikopo kwa watu wasiohusika
wakiwemo watumishi wa Benki hiyo na wafanyabiasgara wengine.
Malengo
makuu ya Benki hiyo ni kutoa mikopo kwa wakulima wa mazaom wafugali
wavuvi na makundi yote yanayojihusiha na kuleta mageuzi katika sekta ya
kilimo.
Naye
Waziri wa Kilimo na Ushirika Mhandisi Charles Tizeba amesema Programu
ya ASDP 11, inakusudia kuongeza eneo la uzalishaji kwa njia ya
umwagiliaji kutoka hekta 450 elfu za awali hadi kufikia milioni 1.
Aidha,
akionyesha baadhi ya Taasisi zilizofanikiwa kuzalisha kwa tija Tizeba
amesema ”Taasisi ya Clintoni imefanikiwa kuzalisha kwa tija katika
shamba la mahindi la hekari moja na kuvuna magunia 1500 kule Mkoani
Iringa”.
Akitoa
vipaumbele vya utekelezaji wa ASDP 11 ni pamoja na usimamizi wa
rasilimali maji na matumizi ya umwagiliaji , ikiwa ni pamoja na
kujiandaa kuzalisha kwa tija hata kama kunatokea mafuriko na ukame.
Kuongeza
dhamani ya mazao kwa kushirikisha kikamilifu sekta binafsi, kuweka
mazingira wezeshi katika sekta kwa kuondoa tozo 98 , kuwa na Sera
zinazotabirikaili kukuza uchumi na kukuza pato la kilimo kutoka asilimia
3.7 hadi kufikia 6 kwa mwaka.
Akiongea
kwa niaba ya nchi wahisani katika Sekta ya Kilimo Mwenyekiti Fred
Kafeero amesema “ Nchi, Mashirika ya Kimataifa na Taasisi zinazochangia
katika programu ya ASDP 11 ni pamoja na Ubelijiji, Uingereza Jumuia ya
Ulaya Ubalozi wa Denmark, Ufaransa, Uswiss, Canada, Uholanzi, Bill and
Melinda Foundation, Benki ya Maendeleo Afrikam, Shirika la Maendeleo la
Ujerumani, Ireland, AGRA, IFAD UNDP. UNIDO, USAID Benki ya Dunia.