Kigwangalla Ashiriki Mazishi Ya Mama Yake Mzazi Hussein Bashe Wilayani Nzega
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge
wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimfariji mbunge wa Nzega
Mjini, Hussein Bashe kufuatia kifo cha mama yake mzazi aliyezikwa jana
wilayani Nzega. Kulia ni mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye. Wabunge
mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na
Abdallah Bulembo walishiriki msiba huo pamoja na viongozi mbalimbali wa
vyama na Serikali.
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge
wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimfariji mbunge wa
Nzega Mjini, Hussein Bashe kufuatia kifo cha mama yake aliyezikwa jana
wilayani Nzega. Kulia ni mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye na mbunge
wa Kigoma Vijijini, Peter Selukamba. Wabunge
mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na
Abdallah Bulembo walishiriki msiba huo pamoja na viongozi mbalimbali wa
vyama na Serikali.
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge
wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa salamu za rambirambi
katika msiba wa mama yake mzazi mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe
aliyezikwa leo wilayani Nzega.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (wa tatu kulia), Waziri wa
Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Hamisi
Kigwangalla (wa sita nyuma kutoka kulia), Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto
Kabwe (wa nne kulia), viongozi wengine wa chama na Serikali na wananchi mbalimbali wakiwemo wa
wilaya ya Nzega wakishiriki kusalia jeneza lenye mwili wa mama yake
mzazi Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (haonekani pichani) muda
mfupi kabla ya kupelekwa makaburini kwa ajili ya maziko wilayani Nzega
jana.
Jeneza lenye
mwili wa mama yake mzazi Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe
(haonekani pichani) likiondolewa kwenye eneo la makaburi kupisha mwili
huo kuhifadhiwa kwenye nyumba yake ya milelel (kaburini) wilayani Nzega
jana.
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (kulia), Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge
wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla (mbele yake kulia) na
viongozi wengine wa vyama na Serikali na wananchi mbalimbali wakiwemo wa
Jimbo la Nzega wakishiriki kumzika mama yake mzazi, Hussein Bashe
katika makaburi wilayani humo jana.