Wema Sepetu: Sina Mpango wa Kurudi CCM
Mrembo
wa Tanzania na Muigizaji Wema Sepetu amemfunga mdomo muigizaji mwenzake
Steve Nyerere kwa kumwambia hana mawazo ya kurudi CCM kama jinsi
ambavyo wengine wanavyofanya.
Wema
amefanya tendo hilo kwa kujibu ujumbe wa Steve Nyerere aliokuwa
ameuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram akimkaribisha ndani ya CCM,
Wakili Alberto Msando ambaye mapema jana alitangaza kujiunga na CCM.
Steve
aliandika "Sasa utakuwa mzalendo wa kweli , Msando naheshimu maamuzi
yako maana ni maamuzi sahihi, kwako pamoja na family yako , rafiki zako
nasi tupo pamoja nawe, soon na yuleeeeeeeee rafiki yetu , dada yetu ,
msanii mwenzetu , naye yupo njiani kurudi nyumbani"
Hata
hivyo Wema Sepepetu baada ya kuona ujumbe huo ambao alihisi kama
inamlenga yeye, alijibu chini ya ujumbe huo kwa kuandika "I hope
hauniongelei mimi... Maana mawazo hayo sina"
Muigizaji
Wema Sepetu alihama ndani ya chama cha mapinduzi Februari mwaka huu kwa
madai kuwa ameamua kujiunga na Chadema kupigania demokrasia ya kweli.

