Mbowe azungumzia watakachofanya sheria mpya vyama vya siasa Ikipita.....
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe amesema iwapo Sheria Namba Tano ya Vyama vya
Siasa ya mwaka 1992 itawasilishwa bungeni wa ajili ya kupitishwa
watakuwa tayari kufa kuliko kukubali ipitishwe.
Akizungumza
jana Jumanne jioni wakati wa kumnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Ibhigi,
iliyopo Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Emmanuel Simba, Mbowe amesema
kama kuna wakati wanaume wanatakiwa kusimama wahesabiwe ni wakati huo.
Alisema
kupitisha sheria hiyo maana yake ni kuingiza ubatili walioufanya ili
uwe sheria kamili, kwamba hakuna mikutano ya vyama vya siasa, hakuna
majadiliano ya mustakabali wa nchi.
"Wanaanda
mkakati wa kubadilisha sheria ya vyama vya siasa taarifa tunayo,
wanataka kuiingiza sheria hiyo kwa nguvu, Sugu(Joseph Mbilinyi)
tunaanzia bungeni, wakati huo ukifika wakituua watuue, wakitunyonga
watunyonge hatutakubali tutaandamana mahali popote," alisema Mbowe.
Mbowe
ambaye ni Mbunge wa Hai alisema watalikataa hilo ili watoto watakaokuja
kesho na keshokutwa wajue baba na mama zao walipambana kulipigania
Taifa lao.
Alisema
Watanzania kwa umoja wao wasilikubali hilo kwa sababu litawanyima haki
kukutana na kujadili wanataka nini kifanyike na watakuwa wamekubali
kurudi nyuma miaka mitano.
Kuhusu
Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyokutana juu na wawakilishi wa vyama vya
siasa , ambapo ilitoa tamko kuwa katika kampeni za uchaguzi wa marudio
ya udiwani, wasijadili masuala ya siasa nje ya kata, jambo ambalo ni la
kipuuzi.
Alisema "tusipokuwa makini na haya matamko ipo siku tutaambiwa wake zetu walale upande huu na sisi upande huu”
"Wanataka mimi mwenyekiti wa chama Taifa nije kujadili masuala ya kata, halafu masuala ya Taifa atajadili nani," alihoji Mbowe.
Alisema
wamezuiliwa kuzungumza na wananchi kwa miaka miwili sasa ndiyo nafasi
pekee waliyopata kuzungumza nao, "Haya ni makatazo ya kipuuzi," alisema.
Mbowe
pia alizungumzia kashfa zinazodaiwa kufanywa na aliyekuwa Mbunge wa
Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu alipokuwa Waziri wa Maliasili na
Utalii, amesema kama wana uhakika na tuhuma hizo wampeleke mahakamani.
"Ilianza
kwa Edward Lowassa alipohamia Chadema, ikaja kwa Fredrick Sumaye na
sasa Nyalandu, kila anayehamia upinzani anaitwa fisadi, sisi hatuogopi
Mahakama kwa sababu tunajiamini, wawachunguze na wawapeleke mahakamani.
"
Nimezungumza na Nyalandu asubuhi ya leo, nikamuuliza kuhusu tuhuma hizo
atachomoa, akasema hilo ni jambo dogo atadili nalo na halimpi shida,"
alisema Mbowe.
