Kilichoendelea Leo Mahakamani Kuhusu Kesi ya Halima Mdee Kumtusi Rais JPM
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kuanza kusikiliza ushahidi wa kesi ya
kumtolea lugha ya matusi Rais John Magufuli inayomkabili mbunge wa
Kawe, Halima Mdee (39), December 7, 2017.
Wakili
wa serikali, Leornad Challo amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria
Nongwa kuwa kesi imeitishwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa lakini
shahidi waliyenaye ana safari.
Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi December 7, 2017 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.
Awali
katika kesi hiyo Mdee aliposomewa maelezo ya awali inadaiwa July 3/2017
akiwa Makao Makuu ya Chadema, maeneo ya Ufipa alitoa lugha ya matusi
dhidi ya Rais Magufuli.
Inadaiwa alitukana kuwa “Rais anaongea hovyo hovyo, inabidi afungwe break”.
Baada
ya kutoa lugha hiyo, July 4/2017 alikamatwa na Polisi maeneo ya
Kibangu, kisha kupelekwa kwa ZCO ambapo alihojiwa na kukiri kutoa maneno
hayo.
Baada
ya kusomewa maelezo hayo, Mdee alikubali wasifu wake ambao ni Jina,
umri, nafasi ya uongozi, mahali anapokaa, kukamatwa na kufikishwa
mahakamani.
Lakini alikana kumtolea lugha ya matusi Rais Magufuli, pamoja kukiri maneno hayo wakati akihojiwa katika ofisi za ZCO.
