Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kuhamia vijijini sasa
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara wakiwa katika baraza la madiwani la kawaida ambapo kwa pamoja wote wameazimia kuhamia katika Makao makuu ya Wilaya ambayo yatajengwa Kijiji cha Nyamwaka kata ya Nyamwaga ili kusogezea wanachi maendeleo ambapo wanachi wa kijiji cha Nyamwaga wametoa hekari 128 bure bila kudai fidia. |
Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Bathromeo Machage katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Moses Misiwa Yomami na anayefuatia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime Vijijini Apoo Castro Tindwa. |
Madiwani wanapitia taarifa. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Moses Misiwa Yomami ambaye pia ni diwani wa kata ya Nyamwaga akisisitiza jambo katikabaraza la Madiwani pia amemwomba mkurugenzi kukutana na watu wa ardhi ili wakutane na kamati ya ulinzi na usalama kwa lengo la kuzungumzia masuala ya migogoro ya ardhi katika vijiji.. |
Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Bathromeo Machage akisisitiza jambo katika Baraza la Madiwani ambapo alisema kuwa kuna haja kubwa ya madiwani kukaa kwa pamoja ili kutatua suala zila la Migogoro ya ardhi. |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Apoo Castro Tindwa akisoma taarifa katika Baraza la Madiwani likiwemo suala la kuhamia Makao mapya ili kufikisjha huduma za wananchi karibu. |