Diamond Platinumz atakiwa kulipa fidia kwa kuiba wimbo

Msondo Ngoma kupitia kampuni ya Mawakili ya Maxim imeitaka Wasafi Clasic Baby (WCB) kuwalipa fidia ya kiasi cha shilingi 300 milioni kutokana na kutumia kionjo hicho cha muziki kilichotungwa na kupigwa katika wimbo wao wa ‘Ajali’ na kukirudia katika wimbo wao wa ‘Zilipendwa’ bila kupata idhini ya mmiliki.
Kionjo hicho kilichotungwa na kupigwa kuanzia dakika ya 6:38 hadi 6:52 kwenye wimbo wa ‘Ajali’ mali ya Msondo Ngoma, kimeigwa na kupigwa katika wimbo wa ‘Zilipendwa’ kuanzia dakika ya 4:55 hadi 5:10.
Barua hiyo imeitaka WCB kulipa fedha hizo ndani ya muda wa siku saba na kama wakishindwa basi Msondo Ngoma watawachukulia hatua zaidi za kisheria.

