Breaking News: Mume wa Irene Uwoya Afariki Dunia
Aliyekuwa
mume wa muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya, mchezaji Hamad
Ndikumana (39) kutoka nchini Rwanda amefariki usiku wa kuamkia leo,
chanzo cha kifo chake kikisemekana ni matatizo ya moyo ambapo jana
alikuwa akiendelea na kazi zake kama kawaida.
Mpaka
anakutwa na umauti alikuwa akicheza katika timu ya APOP Kinyras Peyias
FC ya Cyprus. Alizaliwa Oktoba 5, 1978 na mpaka anafariki dunia
alikuwa ametengana na Uwoya kwa mingi na alikuwa ndiye mkewe waliyefunga
naye ndoa katika Kanisa Katoliki na walibahatika kupata mtoto mmoja
ambaye jina lake ni Krish.