Breaking News " DAVID KAFULILA NAYE AJIONDOA CHADEMA
Mwanasiasa maarufu wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Kigoma
Kusini.Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila leo ametangaza
kujivua uwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kwa kile
alichosema hana imani na vyama vya upinzani kama jukwaa salama la
kupambana na ufisadi nchini Tanzania.
Kafulila amejiondoa CHADEMA na baada ya maamuzi hayo ameeleza sababu
kwamba kwa sasa vyama vya upinzani vinaonekana kupigwa ganzi na kupooza
katika juhudi zake za kupambana na ufisadi na ghafla ufisadi sio agenda
kuu tena ya vyama vya upinzani tena.
“Kwa kuwa sina imani tena na upinzani kama jukwaa salama la kupambana na
ufisadi, nimeamua kwa hiari na utashi wangu kujivua uanachama wa
CHADEMA kuanzia tarehe ya taarifa hii, nitatangaza kwa siku za hivi
karibuni jukwaa jipya la harakati zangu dhidi ya ufisadi”- Kafulila
