UNCDF YAISAIDIA ENSOL KUPELEKA UMEME VIJIJINI
Shirika la
Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (The United Nations
Capital Development Fund-UNCDF), ikishirikiana na kampuni ya Ensol
Tanzania Ltd. (Ensol) wamezindua mfumo wa umeme wa nishati ya jua katika
kijiji cha Mpale kilichopo wilaya ya Korogwe, na hivyo kuwezesha umeme
katika eneo hilo kwa mara ya kwanza.
Mradi huo
ulizinduliwa rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dk.
Juliana Pallangyo ambaye aliipongeza kampuni ya Ensol na washirika wake
ikiwemo UNCDF kwa juhudi zake kubwa za ushawishi wa umeme hasa umeme
mbadala wa jua ili kuboresha ustawi wa jamii na kukuza uchumi wa mtu
binafsi na taifa.
Dk. Pallangyo alisema kwamba serikali ya Tanzania inawashukuru watu wa Ensol kwa juhudi zao kubwa za kupeleka umeme vijijini.
Alisema kwa
Ensol kuweza kufikisha umeme katika maeneo ya ndani kabisa ya kijiji cha
Mpale, kuwaunganisha wananchi na umeme wa saa 24 na wamefanikiwa
kubadili maisha ya wananchi hao.
Alitoa wito kwa jumuiya hiyo kutumia umeme sio kwa kuwasha taa pekee bali pia katika kusukuma mbele kazi za uzalishaji.
Dk. Pallangyo
alifurahishwa na kituo cha afya Mpale kuunganishwa na mfumo wa nishati
ya jua na kuwataka maofisa wa wilaya kulipa Ankara zao kwa wakati ili
kuhakikisha kwamba huduma zinapatikana bila kukoma kwa wananchi.
Kijiji cha
Mpale kipo katika maeneo ya milimani katika kata ya Mpale wilaya ya
Korogwe mkoani Tanga. Kijiji chenye wakazi 9000 na nyumba 730, tangu
kuanzishwa kwake mwaka 1972 hakijawahi kuwa na umeme.
Wengi wa
wanavijiji walikuwa wakitegemea mno mafuta ya taa ambayo kwa kiasi
kikubwa yalikuwa si masafi kwa ajili ya kuwashia taa zao.

Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Juliana Pallangyo akitoa
nasaha wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa
48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale wilayani
Korogwe, mkoa wa Tanga. Kulshoto ni Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa
la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (UNCDF), Peter Malika.
Mreadi huo wa kuunganisha wanakijiji na nishati inayozalishwa kwa nguvu za jua ulianza mwaka 2014 wakati Ensol walipozuru vijiji kadhaa vya mkoa wa Tanga kuangalia uwezekano wa kupata kijiji cha mfano na kubaini kuwapo kwa kijiji cha Mpale.
“Ushirikiano wa UNCDF ulikuwa muhimu katika mradi huu gridi ndogo ya nishati ya jua. Pamoja na kwamba tulipokea fedha kutoka UNCDF na wadau wengine, UNCDF imekuwa ndio chombo cha kuingiza masuala ya kitaalamu na ushauri mwingine. Kushirikiana na UNCDF kumeongeza kuaminika miongoni mwa wadau na taasisi za kifedha,” anasema Prosper Magali, Meneja wa mradi wa Mpale.

Mkuu
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (UNCDF)
nchini, Peter Malika akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa rasmi wa
mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya
jua katika kijiji cha Mpale, wilayani Korogwe mkoa wa Tanga.
Mkuu wa UNCDF Tanzania, Peter Malika alisema kwamba umeme ni chanzo cha maendeleo na kwamba sekta binafsi ina nafasi ya kusaidia serikali katika juhudi zake za kuangaza maeneo ya vijijini.
“Kwa kuwezesha Mpale kuwa na umeme tunawasaidia wananchi wa kijiji hiki kufanya maendeleo ya kiuchumi. Fursa nyingi za kiuchumi zitaibuka, kituo cha afya kitaweza kuboresha huduma zake na wanafunzi watakuwa na muda zaidi wa kusoma.”

Mkurugenzi
Mtendaji wa Ensol Tanzania, Hamisi Mikate akielezea mchakato wa
kufanikisha mradi huo ulivyoenda mpaka kukamilika wakati wa ufunguzi wa
rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya
nishati ya jua katika kijiji cha Mpale wilayani Korogwe, mkoa wa Pwani.
“Wananchi wamefarijika tangu kampuni ya Ensol itembelee kijiji hicho kwa mara ya kwanza na kuzungumza kuhusu uletaji wa umeme wa nishati ya jua. Tumekuwa na ushirikiano mkubwa tangu siku ya kwanza ambapo wamekuwa wakitushirikisha,” anasema Mwenyekiti wa kijiji Augustine Rugambwa.
Bw.Rugambwa aliongeza: “Nimefurahishwa sana kwamba mradi huu umekuja wakati wa uongozi wangu. Ni nafasi adimu ambayo nitaikumbuka maisha yangu yote.
Tunawashukuru sana UNCDF kwa kutukumbuka hata sisi tuliopembezoni. Kupitia Ensol tutaingiza nishati ya umeme majumbani mwetu. UNCDF tunawashukuru kwa msaada wenu huu. Kamwe hatutawasahau.”

Mkurugenzi
wa Miradi wa Ensol na Meneja wa Mradi wa Umeme Mpale, Prosper Magari
akizungumza jambo na kutoa shukrani kwa UNCDF kwa kuwezesha kufanikisha
mradi huo wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme
wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale,
wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga.
“Tunatumia mradi kama huu kama mafunzo. Lengo letu ni kuwa na miradi mingine kama hii 15 katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Tumetembelea maeneo ya nyanda za juu Kusini kuona vijiji vinavyoweza kupatiwa mradi wa umeme wa jua. Tumekubaliana na serikali za mikoa na tawala za mitaa kuwapeleka nishati ya umeme jua na tunatarajia kuwaunganisha na watu nyumba elfu kumi.
Kuna vijiji vingi kama hiki cha Mpale vinavyohitaji umeme, kwa hiyo fursa za umemejua ni kubwa sana!” aliongeza Prosper.
Bw Malika alisema kwamba UNCDF itaendelea kufanyakazi kwa karibu na Ensol na taasisi nyingine za umma na binafsi kuwezesha kufikisha umeme katika maeneo yanayofikika wka shida nchini Tanzania.

Mwenyekiti
wa kijiji cha Mpale, Augustine Rugambwa akisoma risala fupi kwa mgeni
rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa rasmi wa mradi wa
uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua
katika kijiji cha Mpale uliofanyika mwishoni mwa juma wilayani Korogwe,
mkoa wa Tanga.

Kikundi
cha utamaduni Mpale, Millongwe wakitoa burudani wakati wa uzinduzi
rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya
nishati ya jua katika kijiji cha Mpale, wilayani Korogwe, mkoani Tanga.

Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Juliana
Pallangyo (katikati) akishiriki kucheza ngoma ya ‘Mdumange’ ya kabila la
Wasambaa wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mradi wa uzalishaji mdogo
wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha
Mpale, wilayani Korogwe mkoa wa Pwani.

Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Juliana
Pallangyo akifunua kitambaa kuzindia rasmi mradi wa uzalishaji mdogo wa
umeme wa 48KW kwa teknolojia ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale
wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga ambao utasaidia wananchi kuondokana na
changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu. Kushoto ni Mkuu wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (UNCDF),
Peter Malika.


Mgeni rasmi na meza kuu wakitazama wakisoma maneno yaliyoaandikwa kwenye kibao hicho baada ya kuzinduliwa rasmi.

Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Juliana
Pallangyo katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhiria
uzinduzi rasmi mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia
ya nishati ya jua katika kijiji cha Mpale wilayani Korogwe, mkoa wa
Tanga.

Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Juliana
Pallangyo akibadilishana mawazo na Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Mhandisi
Robert Gabriel (kushoto) na Mkurugenzi wa Miradi wa Ensol na Meneja wa
Mradi wa Umeme Mpale, Prosper Magari katika chumba maalum cha kusambazia
umeme katika kijiji cha Mpale mara kuzindua rasmi mradi huo.

Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Juliana
Pallangyo akitembelea chumba cha betri za solar zinazosambaza umeme
katika kijiji hicho.

Mmoja
wa wageni walioshiriki uzinduzi huo akipata huduma ya kunyoa ndevu
baada mradi huo wa umeme wa nishati ya jua kuzinduliwa rasmi katika
kijiji cha Mpale, wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga.

Pichani
juu na chini ni sehemu ya viongozi mbalimbali wa serikali, wananchi wa
kijiji cha Mpale, wafanyakazi wa ENSOL na UNCDF waliohudhuria uzinduzi
rasmi mradi wa uzalishaji mdogo wa umeme wa 48KW kwa teknolojia ya
nishati ya jua katika kijiji cha Mpale wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga.








