Vigogo 6 Jijini Mbeya Kortini kwa Kutafuna Bilioni 5
Aliyekuwa
Mstahiki Meya Mbeya, Athanas Kapunga na wenzake watano akiwemo
aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo Elizabeth Mnuo, Kaimu Mkurugenzi
wa Jiji la Mbeya Dkt Samwel Lazaro wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za
kuingizia hasara serikali.
Viongozi
hao ambao walishamaliza muda wao wamefikishwa mahakamani jana kwa kile
kinachodaiwa kusababisha hasara kwa serikali ya zaidi ya bilioni 5.12
katika kipindi cha uongozi uongozi wao.
Watu
wengine waliofikishwa mahakami ni aliyekuwa mweka hazina wa Halmashauri
ya Jiji la Mbeya James Jirojik, aliyewahi kuwa Mhasibu wa jiji hilo
Tumaini Msigwa na Msimamizi mkuu wa Ujenzi wa Soko la Mwanjelwa Mhandisi
Emily Maganga.
