Ugonjwa wa Manji selo waahirisha kesi yake
Mfanyabiashara
Yussuf Manji (41) anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi pamoja na
wenzake watatu, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu anaumwa na
amepewa mapumziko ya siku mbili.
Hayo
yameelezwa jana Ijumaa, Agosti 18 na Wakili wa Serikali, Esterzia
Wilson mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa.
Wakili
Wilson alidai mahakamani hapo kuwa alipata taarifa hizo za kuwa Manji
anaumwa na amepewa mapumziko ya simu mbili toka kwa askari Magereza.
Hata
hivyo, alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa kutajwa na upelelezi wake
hadi sasa bado haujakamilika. Kesi imeahirishwa hadi Agosti 25, 2017.
Manji
na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba chini ya sheria ya
uhujumu uchumi na usalama wa Taifa kwa kukutwa na vitambaa vya kushonea
sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya zaidi ya Sh200
milioni na mihuri.
Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Deogratius Kisinda (28), Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43).