MBUNGE MATIKO AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI TARIME MJINI.

Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko akiongea na Viongozi wa Dini Mbalimbali Mjini Tarime katika ukumbi wa Ofisi ya Mbunge.






Picha ya Pamoja na Mbune Matiko aliyesimama wa Nne kutoka kulia amevaa sare za Chma na Viongozi wa Dini kutoka Mjini Tarime.
Ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Mhe Esther  Matiko katika kutimiza ahadi zake na kuzungumza na Wanatarime wa Jimbo la Tarime Mjini. Mhe Esther  amefanya mazungumzo na Viongozi wa Dini wote wa Jimbo la Tarime Mjini.

Mazungumzo hayo ya viongozi wa Dini na Mhe Matiko yamefanyika ndani ya Ofisi ya Mbunge wa Tarime Mjini  iliyoko Mtaa wa Kebikiri kata ya Turwa.

Katika mazungumzo hayo  na Viongozi wa Dini, wote kwa pamoja wamempongeza Mhe Matiko kwa kazi kubwa aliyoifanya ndani ya Jimbo lake kwa kuhakikisha anatimiza ahadi zake kuanzia kwenye Elimu, Miundombinu ya Barabara, Kushiriki shughuli za Kijamii katika nyumba za ibada na kwa wananchi wake bila kusahau namna nzuri anavyowawakilisha wananchi wake Bungeni.

Viongozi hao wa Dini hawakusita kutoa ushauri na mapendekezo kwa Mhe Matiko jinsi ya kuwapatia Maendeleo Wanatarime Mjini.
Mchungaji Oluwochi kutoka kanisa na Anazaleti  alieleza kero kubwa wanayokutana nayo ndani ya Hospital ya Bomani hasa upande wa huduma ya Mama na Mtoto, Wajawazito.

Mchungaji Nyangi wa Kanisa la Menonight alieleza na kutoa mapendekezo yake kwa Mhe Mbunge kuwa na mkakati mzuri wa kupanga Mji wa Tarime na zoezi la Kupima Viwanja kwa wananchi liwe linakamilika kwa wakati ili wanachi waweze kuendelea na Majukumu yao kwa lengo la kuleta maendeleo.

Shehe Twafiq Salehe wa Msikiti Mkuu wa Ijuma Wilaya ya Tarime alimshukuru Mhe Mbunge kwa hatua kubwa aliyoichukua ya kuzungumza na Viongozi wa Dini na kumshihi kuendelea kupata wakati wa kuzungumza nao mara kwa mara na kumpongeza kwa kazi kubwa anazoendelea kuzifanya.

Naye Mchungaji Nyagabona  kumpongeza Mhe Mbunge kwa kazi kubwa alizokwisha zifanya kwa wananchi wake. Pia alitoa mapendekezo ya kuhakikisha Vifaa vya kutolea huduma Hospital ya Bomani vinapatikana kwani ni hadha kubwa wananchi wa Tarime Mjini kwenda kutafuta vifaa hivyo nje ya Hospital. 

Akizungumza na viongozi hao wa Dini na kujibu yote yaliyokuwa yamezungumzwa Mhe Matiko aliwahakikishia viongozi hao kuyafanyia kazi yote waliyopendekeza kwa Maendeleo ya Wanatarime. 

Upimaji wa Viwanja ndani ya Jimbo la Tarime Mjini Mhe Matiko alisema, "Upimaji wa Viwanja kwa sasa utafanyika kwa haraka na kasi sana na itakuwa ni njia ya kunusuru Migogoro ya ardhi kwa Wanatarime na tayali jambo hilo nmeshalisemea Bungeni na serikali wameniahidi kutoa ushirikiano wa kutosha hasa kwenye Vitendea Kazi na Wataalamu"alaisema Matiko.

Viongozi hao wa Dini wote kwa pamoja walimuombea Mhe Mbunge Sala ya pamoja kwa Mwenyezi Mungu kuendelea kumlinda na kumtia nguvu aendelee kuwatumikia wanatarime Mjini kwani bado wanamuhitaji sana kwa Maendeleo ya Tarime.

"Taifa lenye Haki ndilo lenye kuwa na Amani". Haya ndiyo maneno aliyoachiwa Mhe Matiko na Viongozi hao wa Dini na kumuombea kuwa na Maneno yenye Hekima pale atakaposimama na kuwazungumzia wananchi wake mahala popote pale.






Powered by Blogger.