Mahakama yaruhusu mkutano mkuu wa club ya simba kufanyika Agosti 13
Mahakama
ya hakimu mkazi Kisutu imetupilia mbali ombi la bodi ya wadhamini wa
klabu ya Simba la kutaka kuzuia mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliopangwa
kufanyika August 13 mwaka huu.
Hakimu
Mkazi amesema haitokua busara kuzuia mkutano huo kwani Agenda za
mkutano hazionyeshi kama kuna agenda ya mabadiliko ya mfumo kama
ambavyo wadhamini wanadai.
Pia
Mahakama imesema sio busara kuzuia Mkutano kwani tayari baadhi ya
wanachama wa Simba wanaoishi mikoani wameshawasili hivyo kuzuia mkutano
huo ni kuwatia hasara, lakini pia uongozi wa klabu umeshafanya
maandalizi.
Na
mwisho kabisa mahakama imesema kwa kuwa mlalamikaji ambae ni Mzee
Kilomoni ana haki ya kuhudhuria Mkutano Mkuu ni vema akaenda kwenye
mkutano huo akaeleza maoni yake.
