Korea Kaskazini: CIA wamepanga kumuua Kim Jong-un
Serikali
ya Korea Kaskazini imesema kuwa imepata taarifa kutoka wizara ya ya
mambo ya ndani yaKorea Kusini kuwa mawakala wa kundi la kigaidi
linaloungwa mkono na Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na shirika la
ujasusi la Korea Kusini wameingia nchini humo kwa lengo la kumuua rais
wa nchi hiyo.
Korea Kaskazini imesema kuwa kabla ya kutekelezwa kwa azmio hilo itahakikisha inawasaka mawakala hao na kuwaangamiza bila huruma
Imeyasema hayo wakati wasiwasi ukiongezeka kati ya Marekani na Korea Kaskazini dhidi ya tuhuma za matumizi ya silaha za nyuklia.
Aidha,
shirika la habari la Korea Kaskazini limesema kuwa njama hiyo
inahusisha kutumiwa kwa silaha kali ya bio-kemikali pamoja na kemikali
yenye miale ya sumu.
Hata
hivyo, mwishoni mwa wiki, Rais Marekani Donald Trump alisema anatamani
kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, ili waweze kufanya
mazungumzo.
