Kikwete Awatetea Wapinzani......Ataka Wasichukuliwe kama Maadui
Rais
mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya
Mrisho Kikwete amevitaka vyama tawala barani Afrika kutovichukulia vyama
vya upinzani kama maadui wa serikali badala yake vionekane kama moja ya
nguzo muhimu katika kutimiza utawala wa sheria.
Aidha,
Rais Kikwete amewataka wabunge wa vyama tawala pamoja na viongozi
wengine, kuvikosoa vyama vyao pale vinapokwenda mrama badala ya kuwa
waoga na kuunga mkono mambo yote.
Rais
Kikwete ambaye ni maarufu Tanzania kwa jina la JK ameyasema hayo
alipokuwa katika mkutano wa masuala ya uongozi barani Afrika wa mwaka
2017 (African Leadership Forum 2017) ambao umefanyikia nchini Afrika
Kusini.
Viongozi
wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Rais mstaafu wa
Tanzania, Benjamin Mkapa, Rais mstsaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo,
Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki na Rais mstaafu wa Malawi,
Bakili Muluzi.
Akizungumza
katika kongamano hilo la siku mbili lililomalizika Agosti 25, 2017, JK
alisema kuwa, kuvichukulia vyama vya upinzani au wanasiasa wa upinzani
kama maadui, ni kutengeneza uadui ambao hauna ulazima katika nchi za
Afrika.
Kikwete
alisema kuwa vyama vya upinzani katika nchi nyingi za Afrika vina kazi
kubwa ya kuhakikisha vinanadi sera zao kwa wananchi ili viweze
kufahamika zaidi kwa vingi ni vichanga. Hii itasaidia wananchi kuwa na
uelewa wa sera pamoja na mipango yao inapofika wakati wa uchaguzi
wakiomba dhamana ya kuongoza nchi, alisema JK.
Mbali
na wito huo kwa watawala, Rais Kikwete alivitaka vyama vya upinzania
pia kukubali matokeo ya uchaguzi endapo umefanyika katika mazingira ya
haki, uhuru na uwazi.
Kazi
ya vyama vya upinzani ni kuhakikisha kuwa serikali inakuwa macho muda
wote kutekeleza majukumu yake, lakini na wao wasiwe watu wa kupinga au
kukataa kila jambo.
Kauli
hii ya Rais Kikwete imekuja wakati ambao vyama vya upinzani nchini
vinalalamika kuhusu kuzuiwa kwa mikutanao ya kisiasa, maandamano, pamoja
na kukamatwa mara kwa mara kwa viongozi wa vyama vya upinzani.