Eneo la Maonyesho ya nanenane Dodoma sasa kujengwa viwanda
Eneo la maonyesho ya nanenane lililopo Nzuguni nje kidogo ya mjini wa Dodoma litamegwa kwa ajili ya kuanzisha viwanda.
Uamuzi
huo umetangazwa leo Jumanne na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jodarn Rugimbana
wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa.
"Tutagawa eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 400 kwa ajili ya viwanda na litakalobakia litatengenezwa uwe uwanja wa kimataifa,"amesema.
Amesema
katika maonyesho yaliyomalizika wiki iliyopita ambayo yamesimamiwa na
mkoa baada ya kuondolewa kwenye usimamizi wa Chama cha wakulima (Taso)
wamefanikiwa kukusanya Sh 226 milioni.
