DYABALA SASA ACHUKUA UZI WA DEL PIERO, NI BAADA YA KUACHANA NA ULE WA ZIDANE, POGBA
Mshambuliaji nyota Juventus, Paulo Dybala sasa anafuata nyayo za gwiji la klabu hiyo, Alessandro Del Piero.
Dyabala ameamua kuachana na jezi namba 21 iliyokuwa maarufu baada ya kutumiwa na Zinedine Zidane na baadaye Paul Pogba.
Sasa
anaingia katika namba 10 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Del Piero
anayeaminika ndiye kipenzi zaidi cha mashabiki wa klabu hiyo katika
karne ya 21.
