Watu wawili wafariki dunia wakibatizwa........Jeshi la Polisi Lamtia Mbaroni Mchungaji
Watu wawili wamefariki dunia kwa kuzama katika mto Ungwasi wakati wakiwa kwenye ibada ya ubatizo.
Kutokana
na tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, linawashikilia watu
watatu akiwamo mchungaji wa Kanisa la Siloamu wilayani Rombo kwa
uchunguzi kwa madai kuwa waumini hao walizama wakati wakiwa katika ibada
iliyoandaliwa na kanisa hilo.
Kamanda
wa Polisi mkoani humo, Hamis Issah amesema tukio hilo lilitokea juzi
saa saba mchana, kwenye mto Ungwasi uliopo Kijiji cha Keni Kata ya Manda
chini wilayani hapa.
Issah amewataja waliofariki dunia kuwa ni Gasper Utoh (47) na Proches Mrema (30).
Kamanda amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Huruma kwa uchunguzi zaidi.
Akielezea tukio hilo, Mkuu wa wilaya hiyo Agness Hokororo amesema waumini hao walifariki dunia wakati wakibatizwa.