Wananchi Mwanza Wajifungia Ndani Wakiogopa Wahalifu wa Kibiti Waliokimbilia Mwanza..........Polisi Yawatoa Hofu, Yasema Hakuna Mhalifu Atakayesalimika
Wakati
wakazi wa mtaa wa Fumagila Mashariki Kata ya Igoma, Mwanza wakiwa na
hofu baada ya watu wawili wanaodhaniwa kuwa majambazi kukimbia juzi,
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, limesema linaendesha msako mkali
kuwasaka watu hao.
Majambazi hayo yanadaiwa kutoroka Kibiti na kukimbilia Mwanza ambapo juzi majambazi 6 yaliuawa katika mapambano na polisi yaliyodumu kwa masaa mawili.
Hata
hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi ameendelea kuwatoa
hofu wakazi hao kuwa hakuna jambo baya litakalotokea kwani polisi
wamejipanga vya kutosha na wapo kwenye msako kila kona kuhakikisha kundi
lote la uhalifu linatiwa nguvuni.
“Wakazi
hao wasiwe na wasiwasi tumejipanga vya kutosha, hakuna kibaya
kitakachotokea hilo kundi tumeshapata taarifa zao hivyo
tutawasambaratisha wote, kikubwa wananchi waendelee kutoa taarifa na
kushirikiana na polisi kwa watu wanaowatilia mashaka.” Amesema.
Katika
tukio hilo polisi waliua watu sita, kukamata silaha ya SMG AK47,
magazine mbili kila moja ikiwa na risasi 30, risasi 36 za AK 47 ambazo
zikuwa nje ya magazine, risasi moja aina ya rafal, risasi nane za
shortgun.
Silaha
nyingine zilizokamatwa ni bastola nne za kienyeji, sare za jeshi za
nchi jirani, kofia sita za kuziba uso, kitambaa cha kichwani, nusu
kanzu, nguo mbalimbali za kiume, mabegi matatu yaliyokuwa yakihifadhi
silaha hizo, baiskeli mbili, pikipiki moja, unga na dagaa.
Mwenyekiti
wa mtaa huo, William Ngemela jana alisema tukio hilo limetoa elimu
tosha katika mtaa huo na mitaa jirani huku akidai tangu azaliwe hajawahi
kushuhudia tukio kama hilo.
“Hii
ni elimu tosha kwasababu haya yote hatukutegemea kama yanaweza kutokea
kwenye mtaa kama huu, lakini angalia silaha zote na vitu vilivyokamatwa,
kwakweli inatishia amani,” amesema Ngemela.
Mwenyekiti huyo alisema watu hao walikuja mtaani hapo kama waumini wa dini ya kiislamu kumbe walikuwa na mambo yao.
"....
lakini hili limekuwa fundisho kwetu, ni wajibu wetu wote kushirikiana,
mimi ni mwenyekiti mmoja lakini jamii ninayoingoza ni kubwa inapaswa
kutoa taarifa.”
Alisema
tangu lilipotokea tukio hilo juzi, baadhi ya wakazi wa eneo hilo
hawakutoka nje ya nyumba zao, walijifungia wakiogopa kuwa hao
waliokimbia wanaweza kurudi kufanya jambo baya.
Nyumba waliyokuwa wamejificha wahalifu hao ambapo 6 kati yao waliuawa, Wawili wakakimbia