Wakili wa Lissu, Fatma Karume amburuza kortini askari Polisi Aliyemshika Mkono Mahakamani....Anadai Fidia ya Bilioni Moja
Wakili
wa Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria
Tanganyika, Fatma Karume amefungua kesi ya madai Mahakama Kuu ya
Tanzania dhdi ya Inspekta wa Polisi Eugene Mwampondela wa Kituo Kikuu
cha Polisi Dar es salaam.
Fatma
amesema kuwa Inspekta Mwampondela alimshika mkono na kumvuta kwa nguvu
hali iliyomsababishia maumivu makali, hivyo anadai alipwe kiasi cha
shilingi bilioni moja kwa kosa la kumwingilia mwilini mwake na
kumbughudhi kwa kumzuia kufanya kazi yake.
“Aliniambia
kuwa ameagizwa na wakubwa kutoka juu, hivyo namfikisha mahakamani ili
amweleze jaji ni nani aliyemtuma, na mimi sitaki kushikwa shikwa mwili
wangu kwa hiyo naomba anilipe shilingi bilioni moja ili liwe fundisho
kwa wengine,”amesema Fatma.
Fatma
ambaye ni mmoja wa mawakili wa Mbunge wa Singida Mashariki alikumbana
na kadhia hiyo wakati akiwa katika harakati za kumtetea mteja wake ili
aweze kupata dhamana.