TANZIA: Jaji Mstaafu wa mahakama Kuu, Upendo Msuya afariki dunia
Aliyekuwa
Jaji wa Mahakama Kuu ambaye amejiuzulu hivi karibuni, Upendo Msuya
amefariki leo Julai 19 baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa
kiharusi.
Mjomba
wa marehemu, Niva Mbaga amethibitisha tarifa hizi na kusema kwamba
marehemu amefariki akiwa Hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa.
Amesema kwamba shughuli za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es Salaam.
“Amesumbuliwa
kwa muda mrefu na ugonjwa wa kiharusi hivyo akawa anapelekwa hospitali
na kurudi nyumbani zaidi ya miezi mitatu sasa na leo hii amefariki
dunia’’ amesema Mbaga
Amesema marehemu ameacha watoto wanne.