Shule 10 Bora Matokeo Kidato cha 6
Matokeo
ya kidato cha sita kwa mwaka 2017 yametoka leo Jumamosi, Julai 15 huku
shule ya Wasichana ya Feza Girls ikiibuka kinara kwa watahiniwa wake 67
kufaulu kwa kupata daraja la kwanza na la pili.
Shule
nyingine zilizoibuka kidedea katika matokeo hayo ni Marian Boys,
iliyoshika nafasi ya pili, Kisimiri (Arusha) imeshika nafasi ya tatu na
Ahmes (Pwani) imeshika nafasi ya nne.
Shule
nyingine ni Marian Girls (Pwani) iliyoshika nafasi ya tano, Mzumbe
(Morogoro) nafasi ya sita, St Marry Mazinde Juu (Tanga) nafasi ya saba,
Tabora Boys (Tabora) nafasi ya nane, Feza BOYS (Dar es Salaam) nafasi ya
tisa na Kibaha ya Pwani iliyoshika namba kumi.