Rais Magufuli Ampa Pole Mwakyembe
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Dkt. Harrison George Mwakyembe kufuatia kifo cha mkewe Bi. Linah
George Mwakyembe kilichotokea usiku wa tarehe 15 Julai, 2017.
Bi. Linah George Mwakyembe amefariki dunia katika hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Katika
salamu hizo, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na kusikitishwa na
kifo hicho, na amesema yeye na familia yake wanaungana na familia ya
Dkt. Mwakyembe katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
“Nakupa
pole sana Dkt. Mwakyembe kwa kuondokewa na mkeo mpendwa Bi. Linah,
natambua hisia za maumivu ulizonazo wewe na familia nzima, nyote
nawaombea Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape subira na uvumilivu katika
kipindi hiki kigumu cha majonzi.
"Namuombea Marehemu Linah George Mwakyembe apumzishwe mahali pema peponi, Amina” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU