Picha: WATEMI WA KISUKUMA,VIONGOZI WA TAS WAIBUKIA KITUO CHA WATOTO WENYE UALBINO BUHANGIJA - SHINYANGA
Watemi wa Kisukuma Kanda ya Ziwa
Victoria na viongozi wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania(
Tanzania Albinism Society -TAS) wamefanya usafi wa mazingira kisha kula
chakula cha pamoja na watoto wenye ualbino wanaolelewa katika kituo cha
Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.
Watemi hao wakiongozwa na Katibu Watemi
wa Kisukuma Kanda ya Ziwa, Mtemi Charles Balele Itale wa Bujashi wilaya
ya Magu mkoa wa Mwanza walitembelea kituo hicho leo Jumamosi Julai
8,2017.
Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye
Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba alisema chama hicho
kimekuwa na ushirikiano mkubwa na machifu wa kanda ya ziwa hicho kuamua
kushiriki nao katika kufanya usafi wa mazingira katika kituo cha
Buhangija.
“Malengo ya kuja hapa kwanza ni kuunga
mkono serikali ya awamu ya tano kuhusu masuala ya usafi,pili ni kuwapa
ujumbe watoto hawa kuwa wawe na utamaduni wa kufanya usafi hata
wanaporudi kwenye familia zao,tatu tumekuja kula chakula cha pamoja na
watoto hawa ili kuonesha kuwa tuko pamoja nao”,alieleza Temba.
Temba alitumia fursa hiyo kuiomba
serikali kuchunguza utitiri wa mashirika yaliyoanzishwa nchini ambapo
sasa yapo zaidi ya 10 na kufuatilia vituo mbalimbali vilivyoanzishwa kwa
lengo la kuwahudumia watu wenye ualbino hususani watoto kwani sasa vipo
takribani 20 lakini wahusika wa vituo hivyo hawasaidii walengwa.
Temba alisema mashirika mengi yamekuwa
yakijikita katika kupiga vita mauaji ya watu wenye ualbino huku
yakisahau kuwa watu wenye ualbino wanakabiliwa na changamoto nyingi
ikiwemo ukosefu wa elimu na saratani ya ngozi ambayo imekuwa ikiua watu
wengi wenye ualbino.
Katibu Watemi wa Kisukuma Kanda ya
Ziwa, Mtemi Charles Balele Itale wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa
Mwanza alimpongeza mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino
kuwakutanisha pamoja katika kituo hicho.
“Juhudi hizi zinaonesha jinsi tunavyowatambua,tunavyowapenda na
tunavyowajali watu wenye ualbino,kwa hiyo katika nafasi zetu za nyadhifa
mbalimbali tunajitahidi kuelimisha na kuwezesha jamii
iwatambue,iwajali,iwapende na kuwapokea katika jamii na watoto warudi
kwenye familia zao na kuishi kama watoto wengine”,alieleza Mtemi
Balele.
“Nimefurahishwa na taarifa ya uongozi wa kituo hiki kuwa sasa watoto
wameanza kwenda likizo kuwaona wazazi wao,hili ni jambo jema sana,Sisi
machifu tuna jukumu letu ni kuielimisha jamii
iwapokee,iwakubali,isiwanyanyase,isiwanyanyapae hivyo sisi kwa
kushirikiana na TAS tutashirikiana katika kutafikia hayo
malengo”,aliongeza Mtemi Balele.
Awali akizungumza katika kituo hicho,Mwalimu Mlezi wa Shule ya Msingi
Buhangija, Frola Kakutebe alisema kati ya watoto wenye ualbino
140,waliopo katika kituo hicho,72 wameenda likizo na 68 wamebakia
kituoni baada ya shule kufungwa kinyume na miaka ya nyuma ambapo watoto
hao walikuwa hawaendi likizo kuonana na ndugu zao.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Selemani Kipanya aliiambia Malunde1 blog
kuwa,sasa Kituo hicho kimepoteza sifa ya kuitwa kituo bali ni shule
kwani tofauti na siku za nyuma hivi sasa watoto wanaoishi hapo wote
wanasoma shule na wanaishi katika mabweni yaliyopo katika shule hiyo.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Katibu Mtendaji wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS
taifa,Mussa Mussa akizungumza katika kituo/Shule ya Msingi Buhangija
katika manispaa ya Shinyanga.Kulia ni Katibu wa Umoja wa Watemi wa
Kisukuma kanda ya Ziwa, ambaye ni chifu/mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu
mkoa wa Mwanza Charles Dotto Balele.Kushoto ni Mwalimu Mlezi wa Shule ya
Msingi Buhangija, Frola Kakutebe-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1
blog
Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa, ambaye ni
chifu/mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza Charles Dotto
Balele Itale akizungumza katika kituo cha Buhangija.Kulia ni Mwenyekiti
wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba
Mtemi Balele akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Buhangija.
Kushono Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS
taifa, Nemes Temba akifuatiwa na Mtemi Nyamilonda III Mikomangwa Aron wa
Mwanza 'Ng'wanza (katikati),kulia ni Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi
mkoani Simiyu wakiwa eneo la tukio.
Kushoto ni Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani Simiyu,akifuatiwa na
Mtemi Charles Gagambaseni Dogani wa Seke - Kishapu mkoani
Shinyanga,kulia ni Mtemi Charles Lubasha Kimwaga Kaswende wa Luhumbo
mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa,
Nemes Temba akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo aliiomba
serikali kuona umuhimu wa kuwapa nguvu viongozi wa kimila kama zamani
kwani wanazungukwa na watu wengi hivyo kuwa na nafasi kubwa ya kuleta
mabadiliko katika jamii.
Watoto,walimu na maafisa kutoka TAS wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba akizungumza katika kituo cha Buhangija.
Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba akizungumza.
Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba akisisitiza jambo.
Watoto na maafisa kutoka TAS wakiwa eneo la tukio
Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa, ambaye ni
chifu/mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza Charles Dotto
Balele Itale akila chakula na watoto wanaolelewa katika kituo cha
Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.
Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani Simiyu akila chakula na watoto wa
wanaolelewa katika kituo cha Buhangija,ambapo wapo wenye
ualbino,wasiosikia na wasioona.
Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa,
Nemes Temba,Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani Simiyu na Mtemi
Charles Gagambaseni Dogani wa Seke - Kishapu mkoani Shinyanga wakila
chakula na watoto kituo cha Buhangija.
Mtemi Charles Gagambaseni Dogani wa Seke - Kishapu mkoani Shinyanga akila chakula na watoto.
Watemi na Viongozi wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS
wakiendelea kula chakula na watoto katika kituo cha Buhangija.
Mtemi Charles Lubasha Kimwaga Kaswende wa Luhumbo mkoani Shinyanga akila chakula na watoto.
Mtemi Nyamilonda III Mikomangwa Aron wa Mwanza 'Ng'wanza akila chakula na watoto.
Afisa Mahusiano na Habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS)Josephat Torner akila chakula na watoto.
Kushoto ni Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa,Charles
Dotto Balele Itale ambaye ni Mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa
Mwanza akifuatiwa na Afisa Mahusiano na Habari kutoka chama cha watu
wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torne (katikati) na Afisa Programu
kutoka Chama cha watu wenye ualbino Tanzania Severin Edward wakifanya
usafi katika kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Buhangija
manispaa ya Shinyanga.
Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani Simiyu akifanya usafi karibu na choo wa watoto katika kituo cha Buhangija.
Mtemi Nyamilonda III Mikomangwa Aron wa Mwanza 'Ng'wanza akiweka uchafu kwenye ndoo.
Kulia ni Afisa Programu kutoka Chama cha watu wenye ualbino Tanzania
Severin Edward na Mwalimu Mlezi wa Shule ya Msingi Buhangija, Frola
Kakutebe wakifanya usafi katika kituo cha Buhangija.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog